KIUNGO Mshambuliaji Henry Joseph Shindika aliyekuwa anacheza soka
la kulipwa nchini Norway katika klabu ya
Kongsvinger IL Toppfotball amejea nchini juzi
baada ya kumaliza mkataba wake.
Akizungumza
na LENZI YA MICHEZO akiwa katika uwanja wa Kinesi alipokuwa akitazama mazoezi ya Simba,
ambao ndiyo ilikuwa timu yake akichezea kabla ya kujiunga na soka la kulipwa
alisema kuwa yupo nyumbani kwa sasa kwani mkataba wake umamalizika.
“Nimerudi
nyumbani baada ya mkataba wangu kumalizika hivyo hapa nimekuja kuwasalimia
viongozi wangu na wachezaji pia”, alisema Henry.
Pamoja na
majibu yake kutoridhisha, LENZI YA MICHEZO iliendelea kumfuatilia na hatimaye lilimkuta
akifanya mazoezi na wekundu hao leo asubuhi hivyo huenda akasajiliwa katika
dirisha dogo kwani usajili umeshafungwa.
Henry ambaye
alijiunga na Kongsvinger IL Toppfotball Februari, 2009 akitokea klabu ya Simba
yenye makao yake katika mtaa wa Msimbazi na aliitwa timu ya taifa kwa mara ya
kwanza 2006 na aliichezea michezo 24 na kufunga bao moja tu.
Kiungo huyo
ambaye alikuwa akivaa jezi namba mbili akiwa Kongs IL Toppfitball aliifunga
mabao mawili katika michezo 74 aliyochezea.
No comments:
Post a Comment