Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, August 4, 2013

SIMBA ALMANUSRA ILALE LUPANGO NI BAADA YA KUKUBALI SARE YA 1-1 TAIFA NA KOMBAINI YA POLISI

Kikosi cha Simba

Kikosi cha Polisi Kombaini.

Mshambuliaji wa Simba, Betram Mombeki akimtoka mchezaji wa Polisi Kombaini, Magige Machango katika mchezo wa kirafiki uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mshambuliaji wa Polisi Kombaini, Admin Bantu akimtoka mshambuliaji wa Simba, Abdulhalim Humud katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
Mshambuliaji wa Simba Betram Mombeki akishangilia goli aliloifungia timu yake dhidi ya Polisi Kombaini katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Timu hizo zilitoka sare ya 1-1.

 SIMBA jana ilibanwa mbavu na kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Kombaini ya Maafande wa Polisi, katika mechi ya kirafiki iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Machi hiyo ilikuwa ni maalum kwa Simba kukipima kikosi kipya cha Simba, ambacho kimesajiliwa kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom, inayotarajia kutimua vumbi kuanzia Agosti 24, mwaka huu.

Mchezo ulianza kwa kasi lakini Simba ndio waliokuwa wa kwanza kuandika bao kunako dakika ya 19 kupitia kwa mshambuliaji wake mrefu Betram Mombeki, ambaye aliunganisha vizuri pasi ya Sino Agustino.
Kuingia kwa bao hilo kuliizindua timu ya Polisi ambayo ilijitahidi kufanya mashambulizi ya hapa na pale lakini ukuta wa Simba uliokuwa ukiongozwa na Said Masoud 'Chollo', Issa Rashid 'Baba Ubaya', Miraji Adam, Rahim Juma na kiungo mkabaji Jonathan Mkude, ulikaa imara.

Baada ya hapo timu zote zilifanya mashambulizi ya zamu huku kila moja ikifika karibu na lango la mwenzake lakini washambuliaji wa pande zote mbili hawakuwa makini.
Hadi timu zote zinakwenda kwenye vyumba vya kupumzikia, Simba ilikuwa mbele kwa bao hilo moja.
Kipindi cha pili kocha wa Simba Abdallah Kibadeni aliamua kufanya mabadiliko kwa kuwatoa Abadulhalim Humud na nafasi yake kuchukuliwa na Ramadhan Singano, akamtoa Ramadhani Chombo 'Redondo' na kumuingiza Marcel Kaheza, huku Hasan Isihaka akiingia kuchukua nafasi ya Rahim Juma.

Polisi nao waliamua kumtoa Magige Bundala na kumuingiza Ahmed Mohamed.
Mabadiliko hayo yalianza kuinufaisha Polisi ambayo ilifanikiwa kusawazisha bao dakika ya 60 kupitia kwa Nicolaus Kabipe ambaye alipokea pasi ya Bantu Admin.
Dakika 15 baadaye, mchezaji John Kanakamfumo, nusura aifungie timu yake bao, ambapo akiwa amebaki yeye na kipa, alipiga mpira ulioambaa ambaa pembeni kidogo ya goli la Simba na kutoka nje.

Baada ya kosa kosa hizo hakuna timu iliyoweza kubadili matokeo hivyo hadi kipyenga cha mwisho kinapulizwa matokeo yalibaki 1-1.

Vikosi vilikuwa kama ifuatavyo; Simba: Andrew Ntalla, Said Masoud 'Chollo', Issa Rashid, Miraji Adam, Rahim Juma/Hasan Isihaka, Jonathan Mkude, Said Ndemla, Abdulhalim Humud/Ramadhan Singano, Betram Mombeki, Sino Agustino na Ramadhan Chombo 'Redondo'/Marcel Kaheza.

Polisi Kombaini: Kondo Salum, Eliasa Maftah, Simon Fanuel, Yahaya Khatibu, Salim Kiss, Nahodha Salum, Magige Machango/Ahmed Mohamed, Andrew Bundala, Mokili Lambo, Admin Bantu na Nicolaus Kabipe. 

No comments:

Post a Comment