London,
England
Chelsea ipo
tayari kuongeza dau zaidi kwa Mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney.
Gazeti
la London Evening Standard, limeeleza kuwa Chelsea itatoa ofa nyingine ya
kumsajili Rooney na kwamba inaandaa pauni milioni 40 (sh. bilioni 96.2 za
Tanzania) kwa nyota huyo wa Kimataifa wa England.
Rooney
bado ni chaguo la kwanza kwa Chelsea katika mpango wake wa usajili wa majira
haya ya joto, na tayari ilishatoa ofa ya pauni milioni 27 ambazo zilikataliwa
mwezi uliopita.
Kwa
sasa Chelsea ina washambuliaji Fernando Torres, Romelu Lukaku na Demba Ba,
lakini Jose Mourinho anamtaka Rooney akaongoze safu hiyo.
@@@@@@@@@
Gerrard:
Suarez akitua Arsenal ataua bendi
Liverpool: NAHODHA wa Liverpool, Steven Gerrard amesema itakuwa ni
majanga kama Luis Suarez ataamua kujiunga na Arsenal mwezi huu.
Gerrard
aliiambia Liverpool Echo: “Kama atakwenda Arsenal, ni wazi ataufanya msimu wetu
kuwa mgumu, ataiimarisha na kuwafanya wapinzani wetu ambao tunawania nao nafasi
ya nne kuwa imara."
@@@@@@@@
Guardiola
aiongoza Bayern kuua
Munich:
KOCHA wa Bayern Munich, Pep Guardiola
ameiongoza timu yake kuifunga Sao Paulo kwa mabao 2-0 kwenye kinyang'anyiro cha
Kombe la Audi na hivyo kuifuata Manchester City katika fainali itakayopigwa
Uwanja wa Allianz Arena wiki hii.
Mabao
ya Bayern yalipatikana kipindi cha pili kupitia kwa Mario Mandzukic aliyefunga
la kwanza na Mitchell Weiser wakati ambapo Rogerio Ceni alikosa penalti kwa
upande wa Sao Paulo. Bayern sasa itakutana na City ambayo iliifunga AC Milan
5-3.
@@@@@@@@@
Adebayor, Defoe hatihati Spurs
London:
MUSTAKABALI wa baadaye wa washambuliaji
wa Tottenham, Jermain Defoe na Emmanuel Adebayor katika kikosi hicho, upo
mashakani kutokana na ujio wa Mshambuliaji wa Valencia, Roberto Soldado.
Gazeti
la 'The Daily Mail', limeeleza kuwa Andre Villas-Boas anamuona Soldado, 28,
kama mshambuliaji sahihi katika safu hiyo na hivyo mustakabali wa Defoe na
Adebayor kuwa mashakani.
No comments:
Post a Comment