London,
England
SANTI
CAZORLA na Nacho Monreal watakosa safari ya Arsenal kwenda kujiandaa na msimu
mpya mashariki ya mbali, jambo litakalowafanya kuhaha kupata namba katika
kikosi cha kwanza mwanzoni mwa msimu.
Wahispania
hao wemepewa muda zaidi wa kupumzika na Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger
kutokana na kuwa katika michuano ya Kombe la Mabara iliyomalizika jana nchini
Brazil, kwa timu yao kucheza fainali na wenyeji hao.
Wachezaji
wengine wa Arsenal waliripoti mazoezini tangu Alhamisi kabla ya wiki hii
kusafiri kwenda barani Asia kwa mechi nne za kirafiki.
Lakini
Cazorla na Monreal hawatajiunga na wenzake hadi mwanzoni mwa Agosti. Katika
michuano hiyo, Cazorla alicheza mechi dhidi Uruguay na Tahiti, wakati ambapo
Monreal alionekana mara moja tu wakati Hispania ilipoibugiza Tahiti 10-0.
Baada
ya safari hiyo ya Asia, Agosti 3 na 4, mwaka huu Arsenal itacheza dhidi ya
Napoli na Galatasaray, mechi ambazo zitakuwa ni mapema mno kwa Cazorla na
Monreal kucheza.
Bado
itakuwa ni vigumu kwao kukubalika kucheza mechi ya ufunguzi ya Ligi Kuu England
dhidi ya Aston Villa, Agosti 17.
No comments:
Post a Comment