Manchester,
England
DAVID
DE GEA yupo mbioni kuongezewa mshahara wake, ikiwa ni sehemu ya kumpongeza kwa
kuonyesha kiwango bora na Manchester United msimu uliopita.
Kipa
huyo wa Kimataifa wa Hispania, ana mkataba na Man United hadi 2016, lakini si
miongoni mwa wachezaji wanaolipwa vizuri zaidi Old Trafford, kutokana na kitita
chake cha pauni 55,000 anazopokea kwa wiki.
Lakini
uongozi wa juu wa United, unatarajia kukaa chini na wawakilishi wa kipa huyo,
22, majira haya ya joto na kujadili uwezekano wa kupandisha maslahi yake hadi
kufikia pauni 75,000 kwa wiki, ambazo wanaamini zitazima ndoto zake za kutaka
kuhamia Barcelona.
Mhispania
huyo ambaye ndiye kwanza amekiwezesha Kikosi cha Hispania U-21 kutwaa ubingwa
wa Ulaya, alikuwa akihusishwa na Barca kwenda kurithi mikoba ya Victor Valdes,
kabla ya kipa huyo kuamua kuitumikia kwa mwaka mmoja zaidi.
De
Gea ambaye aliigharimu United pauni milioni 17.8 akitokea Atletico Madrid miaka
miwili iliyopita, huduma yake bado inatamaniwa na wakali hao wa Nou Camp,
lakini United ipo makini ikitambua kwamba atapewa nafasi kubwa wakati Valdes
atakapoamua kuondoka.
No comments:
Post a Comment