KIDOGO miaka miwili iliyopita lilikuwa ni jambo lenye ushawishi mdogo sana kwa wengi kuamini kwamba Samuel Eto’o angekataa ofa za klabu kubwa barani Ulaya na kwenda kujiunga na timu isiyofahamika sana huko Dagestan.
Badala yake, bilionea Suleyman Kerimov alipoichukua Anzhi Makhachkala, Januari 2011 alifanya usajili wa nyota kadha duniani ili kuifanya klabu yake kuwa na hadhi kubwa, licha ya kwamba hakufanya hivyo bila ya kuwekeza kwa upande wake.
Dili la kumnunua Eto’o kutoka Inter liliwafanya Nerazzurri kuingiza euro milioni 28 kama ada ya uhamisho na mshambuliaji mwenyewe alinasa mkataba uliokuwa na thamani ya euro milioni 20 kwa mwaka baada ya kodi - dili lililokuwa bora kabisa katika ulimwengu wa soka.
Licha ya kuwa na mshahara mkubwa wa aina hiyo, wiki chache zilizopita, ilibainishwa kwamba wawakilishi wa Eto'o, walikutana na rais wa klabu ya Besiktas, Serdal Adali, kuzungumzia mpango wa mshambuliaji huyo wa Cameroon kuhamia Istanbul.
Uhamisho huo si kwamba unaonekana kukwama, kwa kuwa Adali alifeli kwenye kampeni zake, lakini umeibua swali zito kama miamba hiyo ya Uturuki itaweza kuendana na mshahara anaotaka mshambuliaji huyo, unaopita hata anaopokea Cristiano Ronaldo kwenye klabu ya Real Madrid wa euro milioni 13 kwa mwaka kabla ya kodi.
Ni jambo gumu kuamini kama Eto’o atapokea mshahara mkubwa wakati atakapotua Besiktas, lakini je, ule mshahara wake wa Anzhi aliutendea haki? Zaidi ya yote, kila kitu kimekwenda kinyume na kuwa tofauti na Warusi hao walivyodhani hadi kufikia hadi sasa.
"Tunataka kuwa kama Barcelona, wao wanavutia sana," alisema Eto'o baada ya uhamisho wake kukamilika 2011.
"Lengo la Anzhi ni kufikia mafanikio fulani na mambo mengine ya aina hiyo, licha ya kwamba falsafa za kucheza soka safi na kuweza kung'ara katika ulimwengu wa soka. Ipo hivyo."
Hilo lilikuwa lengo zuri, lakini je, jambo hilo limefikiwa. Kumaliza nafasi ya tatu kwenye ligi ya msimu uliopita, limewafanya kufeli kwenye mpango wao wa kucheza Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, huku kipigo cha penalti walichokumbana nacho kwenye mechi ya Kombe la Urusi dhidi ya CSKA Moscow kimetibua zaidi.
Kumekuwa na kufeli kwa uvumilivu kwa mashabiki wa Anzhi pia. Mabango katika mechi ya fainali ya Kombe la Urusi, yalikuwa swali zito kwa kocha Guus Hiddink, akibezwa kutokana na kikosi chake baada ya kushindwa kufikia mafanikio yaliyotarajiwa.
Licha ya klabu kushindwa kutwaa taji kwa mara nyingine msimu huu, kwa namna walivyomalizia msimu wao wa Ligi Kuu Urusi imebainisha mafanikio mazuri kwao katika historia ya klabu yao - huku Eto’o akiwa sehemu kubwa ya mafanikio hayo.
Mshindi huyo mara nne wa tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika amekuwa akifunga mabao kwa kipindi chote alichokuwa na miamba hiyo ya Dagestan.
Nahodha huyo wa Anzhi alifunga mabao 21 katika michuano yote ya msimu uliopita na miongoni mwa mabao hayo, yakiwamo yenye ubora zaidi.
Kama kulikuwa na wasiwasi au hofu yoyote kuhusu uwezo wa Eto’o, kwa kiwango kile alichokionyesha wakati alipowalamba chenga mabeki wanne wa AZ kabla ya kumchambua kipa katika ushindi wa mabao 5-0 kwenye michuano ya Europa League, uliweza kudhihirisha kwamba mchezaji huyo bado anamiliki ujuzi wa aina yake.
Bila shaka, kama Anzhi itahitaji kutwaa taji kwa msimu ujao, mshambuliaji huyo wa Cameroon anapaswa kubaki kwenye kikosi hicho ili kukifanya kuwa tishio baada ya kuondoka kwa beki Christopher Samba katika uhamisho uliofanyika Januari, mwaka huu.
Lakini, pamoja na uhodari wa Eto’o ndani ya uwanja, wachezaji wengine wa timu hiyo wanapaswa kupandisha viwango vyao vya soka ili kuifanya klabu hiyo ya Makhachkala kuwa tishio.
Utajiri wa Kerimov ni jambo linaloifanya timu hiyo kuwa na uhakika mkubwa wa kuwa na mipango wanayotaka na kuweza kuitimiza.
Masuala ya milipuko ya mabomu yanaonekana kutishia hali ya amani na jambo hilo linaweza kutibua kila kitu na Eto’o ambaye alisaidia kwa kiasi kikubwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Lokomotiv Moscow na kushika nafasi ya tatu kwenye ligi kufikiria kuondoka.
Bosi Kerimov amekuwa akitumia fedha nyingi sana, kwa mfano ule wa kumnunulia gari aina ya Bugatti Veyron mkongwe wa Brazil, Roberto Carlos kama zawadi yake baada ya kutimiza umri wa miaka 38. Mambo kama hayo na mishahara ya kama euro milioni 183 kwa mwezi, jambo hilo linaweza kuonyesha bayana kwamba klabu hiyo imejengwa katika misingi ya kifedha zaidi.
No comments:
Post a Comment