Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, May 3, 2013

VYUO VIKUU MBEYA KUSHINDANAJUMAPILI KUTAFUTA BINGWA WA MCHEZO WA POOL TABLE

Mwenyekiti wa chama cha Pool Mkoa wa Mbeya, Aron Samweli (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo vya mashindano ya Safari Lager Pool Higher Learning Mkoa wa Mbeya .Kulia ni Makamu Mwenyekiti , Obmark Malebeja.
Mwenyekiti wa chama cha Pool Mkoa wa Mbeya, Aron Samweli (kulia) akimkabidhi fulana mwanafunzi wa Chuo cha Mzumbe Mkoani Mbeya,Kelvin Mwita kwa ajili ya mashindano ya Safari Lager Pool yanayotarajiwa kuafanyika jumapili

Mwenyekiti wa chama cha Pool Mkoa wa Mbeya, Aron Samweli (kulia) akimkabidhi fulana mwanafunzi wa Chuo cha TIA Mkoani Mbeya,Steven Kiasi kwa ajili ya mashindano ya Safari Lager Pool 

Mwenyekiti wa chama cha Pool Mkoa wa Mbeya, Aron Samweli (kulia) akimkabidhi fulana mwanafunzi wa Chuo cha MUST Mkoani Mbeya,Mwita Masasi kwa ajili ya mashindano ya Safari Lager Pool 

Mwenyekiti wa chama cha Pool Mkoa wa Mbeya, Aron Samweli (kulia) akimkabidhi fulana mwanafunzi wa Chuo cha TEK Mkoani Mbeya,Msuda Jeremia  kwa ajili ya mashindano ya Safari Lager Pool 


MASHINDANO ya mchezo wa Pool Table kwa vyuo vikuu mkoani Mbeya yanafanyika leo kwenye Viwanja vya CCM Iloma

Jumla ya Vyuo vikuu vinne vilivyopo Mbeya vitashiriki ambavyo ni ni Mzumbe tawi la Mbeya, Chuo cha Uhasibu (TIA), Chuo cha Ufundi (TEK) na MUST na  vimeshakabidhiwa vifaa vya mashindano.

Akizungumza na LENZI YA MICHEZO kwa njia ya Simu toka Mbeya, Mwenyekiti wa chama cha mchezo wa Pool mkoa wa Mbeya(MRPA), Aron Samweli amesema kuwa mashindano hayo yatakayoshirikisha vyuo vikuu vinne ambavyo ni Mzumbe tawi la Mbeya, Chuo cha Uhasibu Mbeya, Chuo cha Ufundi na MUST.

“Mashindano ya pool yataanza kesho na vyuo vikuu vya Mzumbe tawi la Mbeya, Chuo cha Uhasibu Mbeya, Chuo cha Ufundi na MUST ndio vitakavyoshiriki na vimeshachukuwa vifaa vya mashindano “, alisema Samweli

Pia amesema chuo kitakachobeba ubingwa wa mkoa huo ndicho kitakacho shiriki katika fainali za taifa za mashindano hayo zitakazofanyika Juni mosi, mwaka huu jijini Dar es salaam.
Bingwa wa mashindano hayo kwa upande wa timu katika ngazi ya mkoa atajinyakulia fedha taslim Sh.500,000, mshindi wa pili Sh.300,000, mshindi wa tatu Sh.200,000 na mshindi wa nne Sh.100,000.

Kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja (wanaume) bingwa atazawadiwa Sh.150,000 na mshindi wa pili Sh.100,000 wakati kwa upande wa wanawake bingwa atapewa Sh.100,000 na mshindi wa pili Sh.50,000, zawadi zote zinatolewa na Safari Lager ambao ndio wadhamini.

No comments:

Post a Comment