Mashindano
ya mchezo wa pool table kwa vyuo vikuu yataanza kutimua vumbi kesho mjini Iringa na yatafanyika
kwenye Ukumbi wa Twisters Club.
Jumla ya
Vyuo vikuu vinne vilivyopo Iringa vitashiriki ambavyo ni Ruaha, CDTI, Mkwawa na
Tumaini na vimeshakabidhiwa vifaa vya mashindano.
Akizungumza
na LENZI YA MICHEZO kwa njia ya Simu toka Iringa, Mwenyekiti wa chama cha mchezo wa Pool mkoa
wa Iringa (IRPA), Salim Kisaku amesema kuwa mashindano hayo yatakayoshirikisha
vyuo vikuu vinne ambavyo ni Ruaha, CDTI, Mkwawa na Tumaini.
“Mashindano
ya pool yataanza kesho na vyuo vikuu vya Ruaha, CDTI, Mkwawa na Tumaini ndio
vitakavyoshiriki na vimeshachukuwa vifaa vya mashindano ambavyo ni pool table,
na vifaa vyake vyote na fulana na kofia ambazo watavaa washiriki”, alisema
Kisaku
Pia amesema chuo
kitakachobeba ubingwa wa mkoa huo ndicho kitakacho shiriki katika fainali za taifa
za mashindano hayo zitakazofanyika Juni mosi, mwaka huu jijini Dar es salaam.
Kwa upande
wa mchezaji mmoja mmoja (wanaume) bingwa atazawadiwa Sh.150,000 na mshindi wa
pili Sh.100,000 wakati kwa upande wa wanawake bingwa atapewa Sh.100,000 na mshindi
wa pili Sh.50,000.
No comments:
Post a Comment