KIUNGO mshambuliaji wa Kimataifa aliyekuwa akiichezea Simba, Patrick Mutesa Mafisango, leo anatimiza mwaka mmoja tangu alipofariki dunia Mei 17, mwaka jana, kwa ajili ya gari iliyotokea Barabara ya Chang’ombe , jijiji Dar es Salaam.
Mafisango yalimkuta umauti akiwa njiani kurejea nyumbani kwake akitoka disko na mwili wake kwenda kuhifadhiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Kifo cha kiungo huyo kilitokea ikiwa ni baada ya siku 11 tangu Simba ilipochukua ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, iliyohitimisha mechi ya mwisho kwa kuifunga Yanga mabao 5-0, iliyochezwa Mei 6, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mafisango aliyejiunga na Simba, akitokea Azam FC na kabla ya kutua nchini aliwahi kuichezea APR ya Rwanda, alikuwa ni mchezaji muhimu katika klabu hiyo.
Kabla ya kufariki Mafisango alikuwa anajiandaa kwenda Rwanda kuitumia timu yake ya Taifa, baada ya kuitwa na aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Sredojevic Milutin ‘Micho’ kwa ajili ya kushiriki michuano ya kimataifa.
Hata hivyo, Mafisango ataendelea kukumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika klabu ya Simba, aliyeng’ara katika msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara, akiwa ni mapachika mabao na mtengenezaji mzuri wa pasho za mwisho.
Mafisango mechi yake ya mwisho kucheza ilikuwa kati ya Simba na Al- Ahly Shandy ya Sudan ya Kombe la Shirikisho barani Afrika iliyochezwa kwenye Uwanja wa Shandy, ambapo Simba ilitolewa kwa mikwaju ya penalty 9-8, baada ya kutoka sare ya mabao 3-3.
Simba iliweza kuifunga timu hiyo katika uwanjani wake wa nyumbani wa Taifa, Dar es Salaam, ambapo Mafisango aliweza kuifungia timu yake bao moja kati ya matatu yaliyoiwezesha Simba kushinda mabao 3-0.
Mafisango ameacha pengo kubwa katika kikosi cha Simba, kutokana na alikuwa kiungo mzuri, aliyewezesha baadhi ya wachezaji wa timu hiyo, akiwemo Emmanuel Okwi, Haruna Moshi ‘Boban’, Amri Kiemba na Felix Sunzu kuonekana ni wazuri katika kikosi hicho.
Mashabiki wa soka nchini na serikali yao, ikiongozwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Fenella Mukangara, alikuwa ni mmoja waliojitokeza kuuaga mwili wake, katika viwanja vya Chang’ombe, Dar es Salaam.
Mwili wake ulisafirishwa kwa ndege ya kampuni ya KQ kuelekea nchini kwao, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kwa ajili ya maziko ambapo utasindikizwa na wachezaji wenzake akiwemo rafiki yake, Haruna Moshi Boban.
Marehemu alizikwa Mei 21, mwaka jana huko Lemba nje kidogo ya jiji la Kinshasa DRC Congo ambako amepumzishwa katika nyumba ya milele.
Kifo cha Mafisango kilikuwa ni pigo kubwa kwa familia ya soka, hususani kwa timu aliyokuwa akichezea ya Klabu ya Simba.
Hata hivyo, kumbukumbu ya mchezaji huyo wa Simba, imefika wakati Simba kesho watacheza na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Simba watatumia mchezo huo, kama kumwezi mchezaji mwenzao
waliokuwa nao katika kikosi kimoja, Mei 6, mwaka jana, wakati iliposhinda mabao 5-0, katika mchezo wa kuhitimisha msimu wa Ligi
Kuu.
Wachezaji wa Simba wanatakiwa kumwezi mwenzao kwa kuhakikisha
waibuka na ushindi mkubwa katika mchezo huo, ili waweze kulinda heshima yao
baada ya kupoteza ubingwa wa ligi hiyo.
Simba wanatakiwa kumwezi kwa hilo, kutokana na mchango wake wa
kuifunga Yanga mabao 5-0 katika mchezo kama huo, uliochezwa Mei 6, mwaka jana.
Marehemu Patrick Mafisango alizaliwa Machi 30, mwaka 1980 na
ameacha mke na watoto watatu. Tutaendelea kukumbuka daima, Amina.
No comments:
Post a Comment