MWAMUZIKI wa bongo fleva,
Nasib Abdul 'Diamond Platinum' amejigamba kumfunika Ney wa Mitego kwenye
mpambano wao utakaofanyika Dar Live Mei 18, mwaka huu.
Akizungumza na LENZI YA MICHEZO, Diamond amesema anataka kudhihirisha
kuwa muziki wa bongo fleva ni zaidi kuliko hip hop kuliko watu wanavyodhani wao
wanaimba mapenzi tu na kubana pua.
"Nawaomba wapenzi wangu wote waje kwa wingi ili waone
kazi yangu kwani naamini nitafunika na watapata burudani ya uhakika",
alisema Diamond.
Mpambano huo umeandaliwa na kampuni ya YUNEDA inayosimamiwa
na Kahabi Ngwendesha ili kuwapa burudani wakazi wa Dar es Salaam na kusaidia
kuinua kipato cha wasanii
"Mpambano unaitwa ni muziki gani kwa maana ni muziki
gani wenye mashabiki kati ya bongo fleva na hip hop ndio maana tumeamua
kuwaweka Diamond na Ney wa Mitego jukwaa moja", alisema Kahadi.
Pia amesema kwa vile siku hiyo ndio ligi kuu inamalizika,
anawaomba mashabiki wafike Dar Live wakamalizie sherehe za ubingwa kwani
kiingilio ni 10,000 tu na kutakuwepo wasanii wengine watakaosindikiza mpambano
huo.
No comments:
Post a Comment