Yanga ambayo
inafukuzia taji la Ligi Kuu ya Tanzania Baraleo itashuka dimbani kupambana na JKT Ruvu ya
mkoani Pwani kwenye mchezo utakaochezwa uwanja wa Taifa.
Yanga ambao
ni wenyeji katika mchezo huo watahitaji kupata pointi zote tatu ili kuweka
matumaini makubwa ya kuchukua Ubingwa wa bara.
Pia JKT Ruvu
nao watahitaji kupata matokeo mazuri ili
kujinasua kwenye mstari wa kushuka daraja kwani hawako katika nafasi nzuri.
Timu ya
Yanga imejipanga vema kufanya kweli kwani wakifanikiwa kupata pointi zote kutawafanya
wahitaji sare moja tu ili kutangaza ubingwa.
No comments:
Post a Comment