Bondia Djamel Dahou akipambana na Hamis Ajali kwenye pambano Ubingwa wa Afrika UBO uzito wa Light Welter Weight lililofanyika ukumbi wa DDC Keko jijini Dar es Salaam jana |
Hapa wanaonyeshana uwezo wa kurushia makonde |
Wamesimama kuimba Wimbo wa taifa la Algeria |
Wimbo wa taifa la Tanzania unaimbwa |
Bondia Djamel Dahou akisujudi baada ya kushinda kwa KO |
Mwamuzi anamtangaza rasmi kuwa bingwa wa UBO Afrika uzito wa Light Welter Weight |
Balozi wa Algeria hapa nchini Djelloul Tabet (aliyevaa miwani) akiwa kwenye picha ya pamoja baada ya pambano kumalizika. |
BONDIA Hamisi Ajali jana alipigwa kwa technical knockout
(KO) na bondia Djamel Dahou wa Algeria kwenye pambano la Ubingwa wa Afrika
Light Welter Weight la raundi 10, lililofanyika kwenye Ukumbi wa DDC Keko,
jijini Dar es Salaam.
Ajali alikumbana na kadhia hiyo kwenye raundi ya pili
baada ya kupigwa konde lililompeleka chini na kushindwa kusisima ndipo Djamel
Dahou alipojichukulia mkanda wa UBO ndani ya dakika nne tu.
Kitendo cha bondia Ajali kupigwa kwa KO kwenye hatua za
awali kilionyesha kuwakasirisha mashabiki wa mchezo huo waliokuwa wamefurika
kushuhudia
Alisikika shabiki mmoja akisema kuwa Ajali kuwa amewatia
aibu kupigwa mapema na sasa hawajui waende wapi ili kuupoza machungu kwani ni
mapema, ilikuwa saa tatu .
Awali akizungumza kabla ya pambano hilo kuanza mgeni
rasmi ambaye alikuwa balozi wa Algeria hapa nchini Djelloul Tabet aliwaasa
mabondia kucheza kwa kufuata kanuni za mchezo huo pia aliwakumbusha kuwa
michezo hujenga urafiki.
“Michezo hujenga urafiki hivyo mfuate kanuni mnapokuwa
ulingoni kwani Tanzania na Algeria ni marafiki hivyo na nyie ipo siku mtakwenda
Algeria kucheza”, alisema Tabet.
Kabla ya pambano hilo kuanza yalichezwa mapambano sita ya
utangulizi ambapo Kassim Gamboo alimpiga Shabani Mkala kwa pointi tatu kwa bila
pambano la raundi nne uzito wa Bantaweight na Joseph Mpilimi alimpiga Kaisi
Rashid kwa pointi mbili kwa moja kwenye uzito wa Lightweight.
Naye Haji Juma wa Tanga alimpiga kwa KO raundi ya tano
Mohamed Mzungu kwenye uzito wa Bantamweight la raundi sita na Ibrahim Tamba
alipewa ushindi kwa mpizani wake Doto Kipacha hakutokea ulingoni.
Amos Mwamakula alimpiga Jumanne Mohamed kwa KO raundi ya
pili kwenye pambano la sita uzito wa Light welter na Juma Fundi alimpiga Abuu
Mtambwe kwa pointi tatu kwa sifuri kwenye pambano la raundi nne uzito wa
Bantamweight.
No comments:
Post a Comment