Aliyekuwa
mjumbe baadae katibu mkuu wa chaneta Anna Kibira amechaguliwa tena
kuwa mwenyekiti wa chama cha mpira wa pete (CHANETA) Katika uchaguzi
uliofanyika jioni ya leo hii Mkoani Dodoma , huku msimazi wa uchaguzi huo
akiwa mkuu wa wilaya ya Bahi na aliyekuwa Mtangazaji wa zamani wa ITV Betty
Mkwasa .
Anna Kibira
amemshinda mpinzani wake Shy-Rose Bhanji kwa tofauti ya la kura
40 katika nafasi ya uenyekiti Anna Kibira amepata kura 61 dhidi ya
mpinzani wake Shy-Rose Bhanji ambaye amepata kura arobaini na moja .
grace khatib
ambaye alikuwa hana mpinzani katika nafasi ya mweka hazina alipata kura za
ndio 66 na kura za hapana 16 kati ya kura 82 zilizopigwa Katika
nafasi ya makamu mwenyekiti kulikuwa na wagombea wawili Zainab Mbiro na Agnes
Madasila katika nafasi hiyo Zainabu Mbiro alipata kura 57 wakati mpinzani
wake amepata kura 27
Chama
kiliweza kuaandaa michuano ya mataifa ya Afrika ni wazi kabisa wana changamoto
kubwa ya kufanya japokuwa mara baada ya ushindi Kibira amesema kuwa anataka
kuupeleka mchezo huo mikoani na kwenda kuuimarisha zaidi vijijini .
No comments:
Post a Comment