BARCELONA, Hispania
LIONEL Messi ameweka rekodi nyingine kwenye La Liga msimu huu,
safari hii ni rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi ugenini, baada ya kufunga bao
lake la 24 ugenini, ndani ya msimu mmoja.
Messi aliingia kutokea benchi kwenye pambano dhidi ya Athletic
Bilbao na kuifungia bao la kusawazisha Barcelona kabla ya kumtengenezea Alexis
Sanchez na kufanya matokeo kuwa 2-1, lakini Bilbao walichomoa katika dakika za
mwisho na pambano hilo lilimalizika kwa sare ya 2-2.
Kwa bao hilo Messi amefikisha mabao 44 ya La Liga msimu huu,
huku akiweka rekodi ya kufunga mabao 24 ugenini, na kuvunja rekodi ya Cristiano
Ronaldo, aliyoiweka msimu wa 2011/12.
Bao hilo lilikuwa ni bao la 100 la Messi kwenye ligi akiwa na Barcelona.
Baada ya kuingia uwanjani kwenye pambano la juzi Messi alionekana kurudia
kiwango chake cha kawaida na kumaliza ukame wake wa mechi mbili bila bao.
No comments:
Post a Comment