MKUU wa Kitengo cha Uanachama wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Primo Corvaro aliwasili jana nchini tayari kutatua mgogoro wa Uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuanzia leo.
Afisa Habari wa TFF, Boniface Wambura amesema kwamba Primo aliwasili pamoja na Mkuu wa Kanda hii, Ashford Mamelodi na tayari wameshaanza kazi iliyowaleta ila wameshindwa kuonana na Waziri wa Habari,Michezo,Vijana na Utamaduni, Dr. Fenella Mukangara kutokana na kuwa kwenye vikao vya bunge la Bajeti linaloendelea Dodoma
Pia Wambura amesema ratiba nyingine inabaki kama ilivyopangwa awali kwa siku tatu na ujumbe huo umeanza kukutana na Sekretarieti pamoja na Rais wa TFF na jioni hii utakutana na wagombea uongozi walioathiriwa na uamuzi wa Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF ambao wakiomba FIFA iingilie mchakato huo.
Majina ya wagombea wakaokutana na ujumbe huo na ratiba ni kama unavyoonekana kwenye majedwali yaliyopo chini.
ORODHA YA WALIOATHIRIWA NA MAAMUZI YA KAMATI YA RUFAA
NA.
|
JINA
|
NAFASI ALIYOGOMBEA
|
UAMUZI WA KAMATI YA UCHAGUZI
|
UAMUZI WA KAMATI YA RUFAA ZA UCHAGUZI
|
OMBI LA SHAURI KUANGALIWA UPYA AU UAMUZI WA KUKATA RUFAA
FIFA
|
1.
|
Ahmedi Yahaya
|
Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu
|
Aloipitishwa
|
Aliondolewa
|
Aliomba shauri lake liangaliwe upya
|
2.
|
Mbasha Matutu
|
Ujumbe wa Kamati ya Utendaji (Mikoa ya Shinyanga na
Simiyu)
|
Aliondolewa
|
Aliondolewa
|
Aliomba shauri lake liangaliwe upya
|
3.
|
Farid Salim Mbaraka Nahdi
|
Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF (Morogoro na Pwani)
|
Aliondolewa
|
Aliondolewa
|
Aliomba shauri lake liangaliwe upya
|
4.
|
Eliud Peter Mvella
|
Ujumbe wa Kamati ya Utendaji (Iringa na Mbeya)
|
Aliondolewa
|
Aliondolewa
|
Aliomba shauri lake liangaliwe upya
|
5.
|
Jamal Emily Malinzi
|
Urais wa TFF
|
Alipitishwa
|
Aliondolewad
|
Aliomba shauri lake liangaliwe upya na alikata rufaa FIFA
|
6.
|
Michael Richard Wambura
|
Makamu wa Rais wa TFF
|
Aliondolewa
|
Aliondolewa
|
Alikata rufaa FIFA
|
Date / Time
|
Activity
|
15 Aprili 2013
Saa 12:30 – 03:00
|
Kuwasili kwa wajumbe wa FIFA
|
15 Aprili 2013
Saa 04:00 – saa 05:00 usiku
|
Kikao na Rais wa TFF pamoja na Sekretarieti
|
16 Aprili 2013
Saa 04:00 – 05:00 asubuhi
|
Kwenda ofisini kwa Waziri wa Michezo kwa ajili ya
kumsalimu
|
16 Aprili 2013
Saa 05:30 – 06:30 asubuhi
|
Kukutana na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kupata taarifa ya
uchaguzi
|
16 Aprili 2013
Saa 06:30 – 08:00 mchana
|
Chakula cha Mchana
|
16 Aprili 2013
Saa 08:00 – 12:00 jioni
|
Kukutana na wagombea walioondolewa
|
17Aprili 2013
Saa 03:00 – 05:00 asubuhi
|
Kukutana na Kamati ya Rufa za Uchaguzi ya TFF
|
17 Aprili 2013
Saa 05:30 – 06:30
Mchana
|
Kupewa taarifa zinazohusiana na mchakato wa uchaguzi,
i.e., kesi zilizo mahakamani
|
17 Aprili 2013
Saa 08:00 – 10:00 jioni
|
Kukutana na watu wengine ambao FIFA wanaweza kuomba
kukutana nao
|
17Aprili 2013
Saa 10:30 – 11:00 jioni
|
Mkutano na waandishi wa habari – kushukuru mamlaka na
pande zilizohusika kwa ushirikiano
|
18 Aprili 2013
Saa 10:00 – 12:00 Alfajiri
|
Kuondoka hotelini kwa ajili ya safari
|
No comments:
Post a Comment