Mshambuliaji wa Simba Felix Sunzu akitafuta mbinu za kumtoka mchezaji wa Polisi Moro Nahoda Bakari |
Kiungo mshambuliaji wa Simba Amri Kiemba akiwa na mpira |
Mshambuliaji wa Simba Felix Sunzu akikimbia na mpira huku mabeki wa Polisi Moro wakimkimbiza |
Kikosi cha Simba |
Kikosi Moro |
BAO la
ushindi la winga wa Simba, Mrisho Ngassa lilitosha kwa timu yake kuibuka na
pointi tatu, baada ya kuifunga Polisi Morogoro mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi
Kuu Tanzania Bara, uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Matokeo hayo
yameiwezesha timu hiyo kufikisha pointi 39, huku ikiendelea kubaki katika
nafasi ya nne na Yanga ikiwa tayari imechukua ubingwa wa ligi hiyo.
Katika
mchezo huo uliochezeshwa na Mwamuzi,
Dominic Nyamisana kutoka Dodoma, Polisi ilikuwa ya kwanza kupata bao
katika dakika ya 10 kupitia kwa Bantu Admin aliyefunga kwa shuti la mbali,
ambalo lilikwenda moja kwa moja nyavuni.
Admin
aliweza kufunga bao hilo baada ya kumalizia kazi nzuri iliyofanywa na Mokil
Lambo, ambaye kabla ya kutoa pasi alipokea mpira ulioanzia kwa Basil Abdul.
Katika
dakika ya 15, Ramadhan Singano ‘Messi’ wa Simba alishindwa kumalizia kazi nzuri
iliyofanywa na Haruna Chanongo, baada ya shuti lake kuokolewa na beki wa Polisi,
Nahoda Bakari.
Simba
ilipoteza nafasi nyingine katika dakika ya 19, baada ya Chanongo kushindwa
kufunga aliyepaisha juu shuti lake baada
ya kupokea pasi kutoka kwa winga wa timu hiyo, Mrisho Ngassa.
Katika
dakika ya 27, mvua kubwa ilinyesha katika uwanja huo na kusababisha utelezi uwanjani.
Dakika ya 30,
Simba waliweza kugongeana vizuri, lakini washambuliaji wao walikosa umakini,
ambapo Chanongo alishindwa kumalizia pasi ya mwisho ya Amri Kiemba akiwa ndani
ya eneo la hatari.
Katika
dakika ya 34, Simba ilifanikisha kusawazisha bao kupitia kwa Chanongo, baada ya
kupokea pasi nzuri kutoka kwa Kiemba aliyefunga kwa shuti kali lililomshinda
kipa wa Polisi Kondo Salum.
Kabla ya bao
hilo katika dakika ya 32 Kocha Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelu ‘Julio’
alimnyanyua kwenye benchi mshambuliaji wa timu hiyo, Felix Sunzu kwa lengo la
kutaka kuchukua nafasi ya Abdalah Seseme, lakini Kocha Mkuu wa timu hiyo,
Patrick Liewig alizuia mabadiliko hayo.
Simba
ilipata bao la pili katika dakika ya 47, kupitia kwa Ngassa baada kuunganisha
krosi nzuri ya beki wa timu hiyo, Nassoro Masoud ‘Chollo’ aliyepanda mbele
kusaidia mashambulizi.
Polisi
Morogoro: Kondo Salum, Rogers Gabriel, John Bosco, Abdallah Mfumo, Chacha
Marwa, Nahoda Bakari, Bantu Admin, Mzamil Yasin/Ally Shomary, Mokil Lambo/
Salum Machaku, Basil Abdul/ Keneth Masumbuko na Nicholas Kabipe.
No comments:
Post a Comment