Bakari Mlenge wa Friends Rangers akiwa na mpira |
Halidi Badra akiwa na mpira wakati wa mchezo wa ligi daraja la pili uliochezwa uwanja wa Makurumla jana |
TIMU za Red Coast, Abajalo na Friends Rangers zimefuzu
kucheza hatua ya Kanda ya Dar es Salaam baada ya ligi daraja la pili kumalizika
zikiwa zinaongoza kwenye nafasi tatu za mwanzo.
Ligi Daraja la Pili mkoa wa Dar es Salaam ambayo ilikuwa
inachezwa kwenye ya hatua ya sita bora ilimazika juzi kwa mechi tatu kuchezwa
kwenye viwanja vitatu.
Katika mechi iliyochezwa Makurumla, Friends Rangers iliifunga
Sharif Stars mabao 2-0, mabao hayo yalifungwa na Khatib Kuduku katika dakika ya
12 na Mwenda Athuman katika dakika ya 57.
Uwanja wa Kinesi Red Coast waliibuka na ushindi wa bao 1-0, lililofungwa dakika ya 32
na Rafael Mapunda.
Abajalo nao imefuzu baada ya kuichapa Boom FC mabao 2-0
kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Airwing lakini hata hivyo mechi hiyo
ilivunjika kutokana na wachezaji watatu wa Boom FC kutolewa kwa kadi nyekundu
na wengine kuumia na kushindwa kukidhi sheria 17 za soka.
Red Coast imefuzu kwa
kujikusanyia pointi 11 wakiwa vinara wa ligiikifuatiwa na Abajalo yenye pointi 10
na Rangers ikihitimisha baada ya kujikusanyia pointi 8.
No comments:
Post a Comment