Oscar Shelukindo akicheza pool table
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupiti bia yake ya Safari
lager imetangaza rasmi kudhamini mashindano ya mchezo wa Pool Table kwa vyuo
vya elimu ya juu ambayo yataanza Mei 4, mwaka huu.
Mashindano hayo yanajulikana kama “Safari Lager Higher
Learning Pool Championships” yanafanyika kwa mwaka wa nne sasa na Safari Lager
imekuwa wadhamini wakuu kwa miaka yote na bingwa katika mkoa atapata 500,000,
wa pili 300,000 na 200,000 na mshindi kwa ngazi ya taifa atapata kikombe pamoja
na 2,500,000.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana
meneja wa bia ya Safari Lager Oscar Shelukindo alisema nia ya kudhamini
mashindano haya ni kuhamasisha wanavyuo kucheza mchezo wa pool table ikiwa ni
burudani baada ya shughuli za masomo yao.
Pia alisema michezo ni muhimu kwani hupumzisha akili na
kufanya warudi darasani wakiwa na ari mpya na pia hukutanisha na watu
mbalimbali.
“Michezo mingi hasa pool ni burudani na husaidia akili
kupumzika baada ya masomo na kufanya akili kufikiri upya na kwa ubunifu na
husaidia kuwakutanisha na watu mbalimbali pia husaidia vijana watumie muda wao
vizuri badala ya kujiunga na magenge yanayoweza kupotosha maadili”, alisema
Shelukindo.
Naye Katibu wa chama cha Pool Tanzania (TAPA) Amos Kafwinga
alisema kuwa mashindano haya yataanzia kwa vyuo kushindana katika ngazi ya mkoa
na baadae mikoa yote itashindana katika ngazi ya mikoa na baadae katika ngazi
ya Taifa ili kupata mshindi wa jumla kwa vyuo vyote.
Pia alisema mashindano ya mwaka huu yatahusisha vyuo vikuu
vilivyo katika mikoa ya Morogoro, Dodoma, Iringa, Mbeya, Kilimanjaro, Arusha,
Mwanza na Dar es Salaam na jumla ya vyuo 54 vinategemewa kushiriki
Bingwa mtetezi ni Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT)
cha jijini Mwanza ambao waalichukua ubingwa kwenye fainali zilizofanyika Iringa
mwaka jana na fainali za mwaka huu zitafanyikajijini Dar es Salaam mwanzoni mwa
Juni mwaka huu.
|
No comments:
Post a Comment