TIMU ya Red coast ya Kinondoni juzi iliifunga Sharif Stars
ya Ilala mabao 3-1 kwenye mchezo wa Ligi Daraja la pili mkoa wa Dar es Salaam
uliochezwa Uwanja wa Airwing Ukonga.
Mchezo huo ambao ulikuwa wa ushindani ulishuhudia timu zote
kwenda mapumziko bila kufungana kutoka na safu za Ulinzi za timu zote kuwa
makini katika kulinda goli.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko
na Red coast ikafanikiwa kupata bao la kuongoza dakika ya 55 lililofungwa
na Mwinyi Ally, Ramadahani Said
aliongeza bao la pili dakika ya 78 na mwisho lilifungwa na Idrisa Pandu dakika
ya 90.
Bao la Sharifu Stars lilifungwa na Hassan Kuka dakika ya 65
baada ya kuwazidi mbio walizni wa Red Coast wakidhani kuwa ameotea.
Kwenye michezo mingine iliyochezwa kwenye uwanja wa Benjamin
Mkapa Friends Rangers waliifunga Boom bo 1-0 lililofunga naRashid Khalfan
dakika ya 14.
Abajalo FC ilitoshana nguvu na Day Break bila kufungana
kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Makurumla.
No comments:
Post a Comment