BADO kidogo tu kocha wa zamani wa Liverpool, Rafael Benitez aibuke na ushindi katika mechi yake ya kwanza dhidi ya timu yake hiyo ya zamani Uwanja wa Anfield, lakini mshambuliaji wa Wekundu hao, Luis Suarez akazima ndoto hizo kwa kufunga bao la kusawazisha dakika za lala salama.
Oscar alitangulia kuifungia Chelsea dakika ya 26, lakini Strurridge akasawazisha dakika ya 52 kabla ya Hazard kuifungia The Blues bao la pili kwa penalti dakika ya 57 na Suarez akasawazisha dakika ya 90.
Kikosi cha Liverpool kilikuwa; Reina, Johnson, Carragher, Agger, Jose Enrique, Gerrard, Lucas, Downing/Shelvey dk80, Henderson, Coutinho/Sturridge dk46 na Suarez.
Chelsea: Cech, Azpilicueta, Ivanovic, Luiz, Bertrand, Ramires, Mikel, Mata/Lampard dk90, Oscar/Moses dk83, Hazard/Benayoun dk78 na Torres.
Rufaa ya kifo: Luis Suarez akifunga kwa kichwa bao la kusawazisha kwa timu yake Liverpool dhidi ya Chelsea
Njaa? Suarez alimuuma Branislav Ivanovic kipindi cha pili.
Bao la kwanza: Oscar akiifungia Chelsea bao la kwanza kwa kichwa Uwanja wa Anfield
SPURS WAIBUTUA MAN CITY 3-1 NA KUITENGEA UBINGWA MAN UNITED MAPEMAAAAAA
KLABU ya Tottenham imefufua matumaini ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao baada ya kuitandika mabao 3-1 Manchester City na kuwakatisha tamaa ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu England.
Kiungo wa zamani wa Arsenal, Samir Nasri aliifungia bao la kuongoza Man City dakika ya tano, lakini baada ya hapo vijana wa Andre Villas-Boas wakaigeuzia kibao City.
Kiungo wa zamani wa Arsenal, Samir Nasri aliifungia bao la kuongoza Man City dakika ya tano, lakini baada ya hapo vijana wa Andre Villas-Boas wakaigeuzia kibao City.
Clint Dempsey aliisawazishia Spurs dakika ya kabla ya 57 Jermain Defoe kufunga la pili dakika ya 79 na Gareth Bale kushindilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la City dakika ya 82.
Matokeo hayo yanamaanisha Manchester United wanaweza kujihakikishia ubingwa kesho wakishinda, kwani watafikisha pointi 84 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote.
Kikosi cha Tottenham Hotspur kilikuwa; Lloris, Walker, Dawson, Vertonghen, Assou-Ekotto, Sigurdsson/Holtby dk60, Dembele, Parker/Huddlestone dk61, Bale, Dempsey na Adebayor/Defoe dk71.
Manchester City: Hart, Zabaleta, Kompany, Nastasic, Clichy/Lescott dk90, Toure, Barry, Milner/Kolarov dk46, Tevez, Nasri na Dzeko/Sinclair dk82.

Kitu hicho: Gareth Bale akimtungua Joe Hart na kufanya 3-1
Shuti: Jermain Defoe akiifungia Tottenham bao la pili mbele ya Vincent Kompany
Ufufuko: Clint Dempsey akishangilia bao la kusawazisha aliloifungia Tottenham
Sita Bora ya Ligi Kuu England kabla ya matokeo ya Chelsea na Liverpool
No comments:
Post a Comment