NYON, Uswiss
SHIRIKISHO la Soka Ulaya (UEFA), limemteua mwamuzi wa
Kiingereza, Howard Webb kuchezesha pambano la nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa
Ulaya kati ya Real Madrid na Borussia Dortmund, kesho kwenye uwanja wa Santiago
Bernabeu.
Real Madrid wakiwa nyumbani wanahitaji kuwa kwenye kiwango cha
juu ilikuweza kurudisha mabao 4-1 waliyofungwa kwenye mechi ya kwanza, hii
inamaanisha kwamba, Webb atakuwa na kazi ya ziada hiyo kesho.
Webb amewahi kuchezesha mechi ya fainali ya Kombe la Dunia
2010 nchini Afrika Kusini, kati ya Hispania na Uholanzi, pia mwaka huo huo alichezesha
pambano la fainali ya ligi ya mabingwa kati ya Bayern Munich na Inter Milan.
Kwenye fainali ya Kombe la Dunia, Webb alipondwa kutokana na
kushindwa kumpa kadi nyekundu, Nigel de Jong baada ya kumrukia kifuani Xavi
Alonso.
No comments:
Post a Comment