KIKOSI cha timu ya soka ya Yanga, sasa kimekamilika kwa
asilimia 100 baada ya wachezaji wao waliokumbwa na majeruhi kuanza mazoezi
kujiandaa na mechi yao ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union,
itakayochezwa Mei Mosi, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts alipandwa na presha kutokana
na wachezaji wake wengi kukumbwa na majeruhi wakiwa katika wakati mgumu wa
kuwania ubingwa wa ligi hiyo.
Wachezaji ambao walikuwa majeruhi ni Jeryson Tegete, Juma
Abdul, Khamis Kiiza na Haruna Niyonzima ambao tayari wamerejea kikosini, huku
Didier Kavumbagu na Ladislaus Mbogo wakianza mazoezi mepesi.
Saleh alisema, Kavumbagu alikuwa anasumbuliwa kifundo cha
mguu na Mbogo alikuwa anauguza kidonda baada ya kufanyiwa upasuaji mdogo katika
shavu lake.
“Ni jambo la
kushukuru kwa kuwa wachezaji hao walikuwa ni majeruhi kwa muda mrefu, hivyo
sasa wameanza mazoezi,” alisema Saleh.
No comments:
Post a Comment