Ras Inno Nganyagwa akionesha tuzo ya Kili Music.
Ras Inno akifanya vitu vyake jukwaani katika moja ya matamasha yake.
BENDI ya
mwanamuziki wa reggae nchini, Ras Inno Nganyagwa imekamilika na anatarajia
kuizinduliwaa rasmi mwezi ujao jijini Dar es Salaam.
Ras Inno
ambaye ni mshindi wa tuzo nne za mwanamuziki bora wa reggae Tanzania, amesema
bendi yake hiyo ina wanamuziki 11 na itazinduliwa katika hafla maalumu katika
ukumbi utakaotangazwa hapo baadaye.
Pia amesema nia
ya kuanzisha bendi hiyo ni aweze kufanya kazi zake za muziki katika ufanisi
bora kwani bendi ya kudumu na wanamuziki
wa kudumu hujenga ‘patern’ ambayo ni sawa na wachezaji waliozoeana uwanjani.
“Bendi
hulinda ladha ya nyimbo husikapia show haziwezikubadilika na inasaidia kuwa na uhakika wa kufanya kazi njema nje ya nchi
kwani huleta tija ya kudumu tofauti ukiwa solo, kazi huja kwa msimu kutokana na
mazoea hapa nchini”, alisema
Amesema bendi
hiyo ni mojawapo ya miradi iliyo chini ya usimamizi wa taasisi yake Raggae
Production House ambayo ni mahsusi kwa kupromoti muziki wa reggae, kwa
ushirikiano na wadau wengine miongoni mwa mitindo mingine kwa kuzingatia weledi
“Dhima ni
kuufufua muziki wa reggae hapa nchinisi kwa kuwa umekufa bali kuna mazingira
yanayoufanya uonekane kama haupo na mashabiki wana hamu kubwa nao.”
Pia
amedhamiria kufanya taasisi yake na bendi iwe vyenye hadhi na naamini mwanzo
huu wa mapinduzi utaungwa mkono na wadau wote wenye mapenzi mema.
No comments:
Post a Comment