IKIWA ni miaka takriban tisa (9) tangu kuhukumiwa
kifungo cha maisha jela, Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samweli Manyele amebainisha kuwa Sampuli ya Vinasaba (DNA) za
mwanamuziki nguli Nguza Vicking “Babu
Seya” na watoto wake hazikufikishwa ofisini kwake kwa ajili ya kupimwa.
Profesa Manyele, aliyasema hayo juzi mjini Arusha,
wakati akijibu maswali ya washiriki wa warsha iliyolenga kutoa elimu kwa
wafanyakazi wa idara za upelelezi, ustawi wa Jamii, Mahakama na Wanasheria wa
Sekta binafsi iliyofanyika mjini hapa.
Katika warsha hiyo, Mratibu wa Chama cha Waandishi wa
Habari Mkoa wa Arusha (APC), Seif Mangwangi alitaka kujua kama vipimo vya DNA
vya Babu Seya, watoto wake na mtoto aliyelawitiwa viliyochukuliwa kama
vilifanyiwa kazi na ofisi ya Mkemia Mkuu, ambapo Profesa Manyele alijibu kuwa
Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali haikupokea Vinasaba vya watuhumiwa hao kwa
ajili ya kuvipima.
“Sampuli za Vinasaba hazikuja kwetu, ziliishia kwenye
vyombo vingine vya Serikali. Lakini pia si kila kesi inayosikilizwa lazima
ihitaji vipimo vya DNA,” alisema Prof. Manyele.
Prof. Manyele alisema kwa upande wa kesi ya Babu Seya na
watoto wake ilikuwa na mlolongo wa mambo mengi yaliyokuwa yakiangaliwa ya
kihistoria, hivyo vipimo vya vinasaba vilichukuliwa lakini havikufanyiwa kazi
kama ambavyo inadhaniwa.
“Hata kama tulihitaji DNA, sisi hatulazimishi Mahakama
kutumia vipimo vyetu. Kama upande wao walijiridhisha na ushahidi hilo ni lao
ama pia ushahidi ulijitosheleza,” aliongeza.
“Kesi nyingine zinamalizika kwa upelelezi wa kawaida wa
polisi au hospitali na vipimo vya DNA si vya mwisho vinavyofanya uamuzi wa kesi
uwe A au B,” alisema Prof. Manyele.
Juni
25 mwaka 2004, Babu Seya na wanaye walihukumiwa kifungo cha Maisha jela na
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ambapo aliyekuwa Hakimu Mkuu Mkazi wa mahakama
hiyo, Addy Lyamuya aliwatia hatiani kwa makosa 23 ya kubaka watoto wa kike
wenye umri kati ya miaka sita na minane na kulawiti watoto wa kike wenye umri
kama huo.
Mara
baada ya hukumu hiyo ambayo iliibua simanzi kubwa kwa ndugu, jamaa na wapenzi
wa muziki hapa nchini, Babu Seya na wanaye walikata rufaa katika Mahakama Kuu
ambapo Januari 27 mwaka 2005, aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es
Salaam, Thomas Mihayo aliitupilia mbali rufaa yao.
Katika
rufaa yao, Babu Seya na wanae walikuwa wakipinga hukumu iliyowatia hatiani kwa
makosa 10 ya kubaka watoto wa kike wenye umri kati ya miaka sita na minane na
mengine 11 ya kulawiti watoto wa kike wenye umri kama huo makosa ambayo
walidaiwa kuyatenda kati ya Aprili na Oktoba mwaka 2003, eneo la Sinza kwa
Remmy, Dar es Salaam.
Hata
hivyo katika kupigania haki yao Wasanii hao, walikata rufaa tena katika
Mahakama ya Rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu, Dar es Salaam.
Haya hivyo Alhamisi ya Februari 11, 2010, rufaa yao iligonga
mwamba baada ya kuwaachia huru watoto wawili wa Babu Seya, Nguza Mbangu
(Mashine) na Francis Nguza (Chichi) na kuyatupilia mbali mashitaka 18 kati ya
23 yaliyokuwa yakiwakabili wanamuziki hao kwa maelezo kuwa hayatambuliki katika
sheria za nchi. Mahakama ya Rufaa ilikazia hukumu ya Kifo cha maisha kwa Babu
Seya na mwanaye mmoja Papii Kocha, ambao wanaendelea kutumikia kifungo hicho
katika Gereza la Ukonga, jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment