Rais wa Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amewataka viongozi wa
vyama vya mpira wa miguu vya mikoa kuhakikisha wanaingiza wachezaji wenye umri
sahihi katika michuano ya U15 FIFA Copa Coca-Cola 2013.
Ametoa mwito huo jana wakati akifungua semina elekezi ya michuano ya Copa
Coca-Cola ambayo kuanzia mwaka huu itakuwa ikishirikisha watoto wenye umri chini
ya miaka 15. Rais Tenga amesema hakuna jambo la kipuuzi kama kuchomekea
wachezaji ambao wamezidi umri unaotakiwa kwa vile lengo la michuano ya aina hiyo
ni kubaini vipaji na kuwafanya watoto wapende kucheza mpira wa miguu. “Kwanza
nawashukuru kwa kutenga muda wenu na kuhudhuria semina. Lakini ni vizuri pia
mkahakikisha mnakuwepo kwenye mashindano ili kutekeleza haya ambayo
tutakubaliana katika semina hii. Mkileta mtu mwingine anaweza kutuanzishia mambo
mengine badala ya yale tutakayokubaliana,” amesema Tenga. Pia ameishukuru
kampuni ya Coca-Cola ambaye imekuwa ikidhamini michuano hiyo tangu mwaka 2007
ambapo semina hiyo elekezi inayoshirikisha makatibu wa vyama vya mpira wa miguu
vya mikoa na waratibu wa mikoa wa michezo ya UMISSETA ni ya saba
mfululizo.
Ratiba ya michuano
hiyo kuanzia mwaka huu imebadilika ambapo sasa itaanzia ngazi ya wilaya Aprili
wakati fainali katika ngazi ya Taifa itachezwa Septemba.
No comments:
Post a Comment