WAKICHEZA huko Amman jana Japan walishindwa kuifunga Timu iliyokuwa Mkiani mwa kundi lao, Jordan, na kujikuta wakipigwa Bao 2-1 na hivyo kushindwa kuwa Nchi ya Kwanza Duniani kuweza kufuzu kucheza huko Brazil Mwaka 2014 katika Fainali za Kombe la Dunia.
Jordan ndio waliotangulia kwa kufunga Bao mbili kupitia Khalil Zaid Bani Attiah katika Dakika ya 45 na Farhod Tadjijev, Dakika ya 61 na Japan kufunga Bao lao katika Dakika ya 69 kupitia Mchezaji wa Manchester United, Shinji Kagawa.
Hata hivyo, Japan bado wana Mechi 2 na wanahitaji Pointi 3 tu kwenda Brazil.
Mechi zao zilizobaki ni Juni 4 wakiwa Nyumbani dhidi ya Australia na Juni 11 ugenini na Iraq.
Kwenye Kanda ya Bara la Asia, Timu mbili za juu toka kila Kundi zitaenda Brazil na Timu za nafasi ya 3 za kila Kundi zitacheza Mtoano ili kupata Timu moja itayoivaa Timu ya 5 ya Kanda ya Marekani ya Kusini na Mshindi wa Mechi hii kwenda Brazil.
MATOKEO:
Jumanne Machi 26
Australia 2 Oman 2
Korea Kusini 2 Qatar 1
Uzbekistan 1 Lebanon 0
Jordan 2 Japan 1
MSIMAMO:
KUNDI A
Uzbekistan Mechi 6 Pointi 11
Korea Republic Mechi 5 Pointi 10
Iran Mechi 5 Pointi 7
Qatar Mechi 6 Pointi 7
Lebanon Mechi 6 Pointi 4
KUNDI B
Japan Mechi 6 Pointi 13
Jordan Mechi Mechi 6 Pointi 7
Australia Mechi 5 Pointi 6
Oman Mechi 6 Pointi 6
Iraq Mechi 5 Pointi 5
No comments:
Post a Comment