Kwango cha ubora wa soka la Tanzania
kimepanda kwa nafasi 8 kutoka kutoka katika nafasi ya 127 mpaka kufikia nafasi
ya 119 kwa mujibu wa mabadialiko ya viwango vya ubora vinavyokadiriwa na
shirikisho la soka duniani FIFA. vilivyo tolewa hii leo.
Soka la Tanzania kwa mujibu wa viwango hivyo vya
FIFA katika miaka ya hivi karibuni limekuwa likiporomoka kwa kasi ya kukatisha
tamaa hasa baada ya aliyekuwa kocha wa timu ya Taifa wakati huo Marcio Maximo
kuondoka nchini baada ya kmataba wake kumalizika na nafasi yake kurithiwa na Jan
Poulsen na kisha Kim Poulsen.
Januari 19 mwaka huu Tanzania ilifanikiwa kuichapa
Zambia kwa bao 1-0 kabla ya February 6 kufanikiwa kuitandika Camerron kwa
ushindi kama huko ambao ulipokelewa kwa furaha na mashabiki wa soka nchini kwani
hizo ni miongoni mwa timu vigogo katika soka la Afrika.
Hata hivyo licha ya Tanzania kupata matokeo hayo ya
michezo hiyo miwili bado katikati ya mwezi February FIFA ilitoa viwango vipya
vya ubora wa mataifa wanachama wake ikiwa ni siku tano baada ya kumalizika kwa
fainali ya mataifa ya Afrika nchini Afrika kusini ambapo Tanzania iliporomoka
kutoka nafasi ya 124 mwezi January mpaka kufikia katika nafasi ya
127.
Barani Afrika Tanzania sasa inakamata nafasi ya 33
ikipanda kwa nafasi 4.
Machi 24 timu ya taifa ya Tanzania itakuwa ikishuka
katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kucheza dhidi ya Morocco mchezo wa
makundi kuwania tiketi ya kucheza fainali ya kombe la dunia 2014 nchini
Brazil.
Endapo Tanzania
itafanikiwa kuifunga Morroco katika mchezo huo itakuwa ni fursa nyingine ya
kupanda tena katika viwango vya ubora wa soka lake hasa ikizingaziwa kuwa
Morocco iko juu kiubora ikishika nafasi ya 77.
No comments:
Post a Comment