Baraza la vyama vya soka Afrika mashariki na kati
CECAFA limethibitisha kifo cha aliyekuwa afisa habari wa baraza hilo Finny
Muyeshi ambaye amefariki dunia jana jioni.
Akiongea na Lenzi ya Michezo, Katibu wa baraza hilo
Nicolaus Musonye amesema kuwa baraza lake limesikitishwa na kifo cha afisa
habari wake ambaye amekuwa mchapa kazi hodari ndani ya baraza hilo ambaye
aliugua kwa muda mrefu na hatimaye jana akafariki dunia.
Musonye amesema kuwa mazishi ya Muyeshi yatafanyika
wiki ijayo.
Amesema kwa CECAFA huo msiba mkubwa kwani alikuwa
mstarabu na mwenye kujituma muda wote katika kazi yake na kwamba pengo lake ni
kubwa katika baraza hilo.
No comments:
Post a Comment