Friday, March 15, 2013
LADSLAUS MBOGO WA YANGA AFANYIWA UPASUAJI WA UVIMBE KWENYE TAYA
Mlinzi wa kati wa timu ya Young Africans Ladislaus Mbogo anaendelea vizuri baada ya jana kufanyiwa upasuaji wa uvimbe (shavuni) katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es salaam, upasuaji uliofanyika chini ya usimamizi wa daktari wa timu ya Young Africans Dr Nassoro Matuzya.
Mara baada ya mazoezi ya leo asubuhi katika uwanja wa mabatini Kijitonyama, wachezaji wote wa Young Africans pamoja na benchi la ufundi waliongozana kwenda Hopsitali ya Mwananyamala kumpa pole Mbogo ambaye jana alifanyiwa upasuaji wa uvimbe sehemu ya shavu la kushoto.
Akiongea leo asubuhi baada ya kutembelewa na wachezaji na benchi la Ufundi, Mbogo amesema anajisikia vizuri, anamshukuru mungu upasauji umeenda vizuri na hali yake inaendelea kuimarika hivyo anaamini muda si mrefu atarudi katika hali yake ya kawaida.
Mbogo ambaye alisajiliwa mwaka jana katika msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom 2012.2013 akitokea timu ya Toto Africans, amekifikia hatua hiyo ya kukubali kufanyiwa upasuaji kufuatia kufanyiwa uchuguzi na madakatari kutoka hospital ya Mwananyamala.
Dr Nassoro Matuzya akiongea kwa niaba ya madaktari waliomfanyia upasauaji, amesema upasuaji ulifanikiwa kufanyika salama kabisa, tulimfanyia upasuaji jana asubuhi kufikia mida ya mchana tayari tulikua tumeshamaliza na kwa sasa yupo wodini kwa mapumziko chini ya uangalizi wa madakatari.
Kwa mujibu wa daktari wa Yanga, Dr Matuzya, Mbogo atakua nje ya uwanja kwa kipindi kisichopungua wiki tatu akiendelea kuunguza sehemu aliyofanyiwa upasuaji.
Haruna Niyonzima akiongea na Ladislau Mbogo asubuhi ya leo walipokwenda wachezaji wa Yanga kumjulia hali hospitali
Katika hatua nyingine Kikosi cha Young Africans kimeendelea na mazoezi yake katika uwanja wa mabatini Kijitonyama kujiandaa na mchezo dhidi ya timu ya Ruvu Shooting, mchezo utakaofanyika siku ya jumamosi katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Kikosi cha wachezaji 25 kipo kambini katika hosteli za klabu zilizopo mitaa ya Twiga/Jangwani ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo huo wa jumamosi, mchezaji pekee ambaye hayupo kambini ni Ladislasu Mbogo ambaye amedanyiwa upasuaji wa uvimbe sehemu ya shavuni
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment