Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, March 10, 2013

SIMBA YAMALIZIA HASIRA ZA LIBOLO KWA COASTAL UNION TAIFA LEO BILA NYOTA WAKE

Simba SC leo wamezinduka kuichapa Coastal Union mabao 2-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na kufufua matumaini ya kutetea ubingwa wao kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa leo.

Ushindi huu, unaifanya Simba SC itimize pointi 34, baada ya kucheza mechi 19, na kubaki nafasi ya tatu, nyuma ya Azam FC yenye pointi 37, wakati Yanga SC wapo kileleni kwa pointi zao 45. 
Hadi mapumziko, Simba SC walikuwa mbele kwa mabao 2-0.

Coastal walianza vema mchez, wakisukuma mashambulizi mfululizo langoni mwa Simba na lakini Abel Dhaira aliweza kupangua mashuti ya washambuliaji wa Coastal

Mrisho Khalfan Ngassa aliwainua vitini wana Simba dakika ya kwanza ya muda wa nyongeza, baada ya kumchambua kipa Shaaban Kado, akimalizia pasi safi ya Rashid Ismail.
Haruna Chanongo alipigilia msumari wa pili kwenye ‘jeneza’ la Coastal kwenye dakika ya tatu wa muda nyongeza akimalizia kazi nzuri ya Ngassa, kufuatia shambulizi la kushitukiza.

Kipindi cha pili, Coastal walikianza kwa kasi na kufanikiwa na kupata bao la kufutia machozi dakika ya 50, lililofungwa na kiungo Razack Khalfan aliyeunganisha krosi ya Twaha Shekuwe.
Simba SC ilichelewa kuingia uwanjani na kukosa hata muda wa kupasha misuli, kutokana na matatizo ya kufungiwa hotelini. 

Katika mchezo huo, kikosi cha Simba SC; Abel Dhaira, Nassor Masoud ‘Chollo’, Miraj Adam, Hassan Hatibu, Shomari Kapombe, Jonas Mkude, Amri Kiemba, Rashid Ismail, Abdallah Seseme, Haruna Chanongo na Mrisho Ngassa.

Coastal Union; Shaaban Kado, Hamad Hamisi, Abdi Banda, Mbwana Hamisi, Philip Mugenzi, Razack Khalfan, Daniel Lyanga, Mohamed Athumani, Deangelis da Silva, Suleiman Kassim ‘Selembe’ na Joseph Mahundi


Wachezaji wa Simba wakishangilia bao la kwanza lililofungwa na Mrisho Ngassa wakati wa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Coastal Union uliochezwa uwanja wa Taifa


Mshambuliaji wa Simba Haruna Chanongo akipiga pasi huku beki wa Coastal Union Mbwana Hamis wa Coastal Union wa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Coastal Union

Beki wa Simba Nassor Masoud akimruka golikipa wa Coastal Union Shaban Kado wakati wa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Coastal Union


Beki wa Coastal Union Abdi Banda ( wa kwanza kulia) akiondoa mpira kwenye himaya ya kiungo mshambuliaji wa Simba Amri Kiemba (wa pili kulia) wakati wa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Coastal Union

Beki wa Simba Nassor Masoud akimiliki mpira huku wa golikipa Coastal Union Shaban Kado akimwangalia wakati wa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Coastal Union

No comments:

Post a Comment