Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, March 10, 2013

ARUSHA YANG'ARA KWENYE MBIO ZA NYIKA ZILIZOFANYIKA LEO KILIMANJARO

DICKSON MARWA AKIMALIZA
WANARIADHA WA KILOMETA 12 KATUIKA MBIO ZA NYIKA
WANARIADHA WA KILOMETA 12 WALIPOANZA KUTIMUA MBIO

MBIO za Taifa za Nyika zimefanyika leo, mjini Moshi katika viwanja vya gofu za Moshi Club na kushuhudia wanariadha kutoka katika mkoa wa Arusha wakitawala mbio hizo kwa kuchukua nafasi za mwanzo katika mbio za kilomita 12, 8 na 6 zilizoshirikisha wakimbiaji 100.

Katika mbio za utangulizi za kilomita 6 wanawake , Anjeline Irene 21:19;57, Selina Amosi 21:31:86, Fadhila Salum wote kutoka Arusha mbio za km 8 wanawake Jaeldine Sakilu (JWTZ-Arusha) 27:00:34, Zakia Mrisho (Arusha) 27:24:58 na Catherine Lange (Manyara) 28:12:91.

Katika upande wa wanaume km 8, Dotto Ikangaa 23:53:95 JWTZ-Arusha, Joseph Theophil Mbulu 23:56:41 na Mohammed Ally 24:13:54 JWTZ- Arusha huku mbio za km 12 wanaume akichukua Dickson Marwa 36:34:52 kutoka Holili-Kilimanjaro.

Awali akizungumza na waandishi wa habari mapema kabla ya kuanza kwa mbio hizo, Rais wa Shirikisho la Riadha Taifa, (RT), Anthony Mtaka alisema kuwa madhumuni ya mbio hizo, ni kuandaa kikosi kitakacho iwakilisha Taifa katika mbio za Nyika za dunia zitakazofanyika Machi 24, nchini Poland pamoja na kuibua vipaji vya riadha nchini.

Mtaka amesema kuwa sababu za kuhamishia mbio hizo mkoani Kilimanjaro ni kutokana na mdhamini waliyempta hapo awali kujiondoa na hivyo kuwalazimisha kutafuta mdhamini mwengine ambapo alisema, Executive Solution walisaidia sana.

Rais Huyo amesema kuwa RT kwa sasa inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo la udhamini na kuongeza kuwa mbio hizo kwa mkoa wa Morogoro kujiondoa na hivyo wakalazimika kutafuta namna ya kufanikisha mbio msaada ambao alisema waliupata kutoka kwa uongozi wa mkoa wa Kilimanjaro.

Akizungumzia juhudi za RT kuokoa riadha nchini, Mtaka amesema kwa sasa wameshaanda programu ya kukuza vipaji ambapo alisema kuwa tayari kuna vijana 12 ambao wameshawaombea katika chuo cha polisi ili kuhakikisha wanakuwa pamoja kambini na lengo ni kufuta uteja katika riadha.

Kuhusu tatizo la maandalizi ya timu ya taifa ya Riadha ambapo kwa miaka mingi watu wamekuwa wakiilalamikia RT, Mtaka amesema kuwa wao kama RT hawana timu, wao majukumu yao ni wasimamizi wa timu na kuhakikisha kuwa timu inapata huduma zote kabla ya mashindano.

 Nao baadhi ya wanariadha walioshiriki mbio hizo, Jaeldine Sakilu, aliyeshinda mbio za km 8 wanawake na Dickson Marwa, aliyeshinda mbio za km 12 wanaume, wamesema wako tayari kuiwakilisha nchi katika mbio za Poland lakini walisisitiza umuhimu wa kuwepo kwa maandalizi na ushirikiano kutoka kwa wadau wa Riadha.

Jumla ya wakimbiaji wapatao 100 kutoka katika mikoa ya Mwanza, Arusha, Manyara, Singida, Mara, Zanzibar, mbeya, Dar es salaam na kilimanjaro walichuana jana katika mbio za Nyika za taifa zilizofanyika katika uwanja wa gofu wa Moshi Club ulioko katika Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro ambapo mshindi wa kwanza alipokea zawadi ya Sh. 60,000

No comments:

Post a Comment