Thibaut Courtois amethibitha juu ya matamanio yake ya kuendelea kusalia na Atletico Madrid msimu ujao badala ya kurejea katika klabu yake aliyokulia ya Chelsea ya England.
Raia huyo wa Belgiam katika kampeni ya misimu miwili iliyopita, alikuwa na klabu hiyo yenye maskani yake katika mji mkuu wa Hispania wa Madrid, klabu ambayo ilifanikiwa kushinda mataji mawili ya Europa League na UEFA Super Cup ikiwa ni pamoja na kucheza fainali ya Copa del Rey.
Courtois mpaka sasa bado hajaichezea klabu yake iliyomkuza ya Chelsea ambayo alimsaini kutoka katika klabu ya Genk inayoshiriki ligi ndogo inayotambulika kama Jupiler Pro League mwaka 2011.
Mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 21 ametanabaisha kuwa hana haraka ya kurejea Stamford Bridge na kuwa kama mlinda mlango namba mbili Petr Cech.
Aidha Courtois, ambaye ameweka rekodi ya kucheza dakika 820 bila kuruhusu goli kabla ya mchezo wa Jumapili ambapo walipoteza dhidi ya Real Sociadad kwa bao 1-0, amesema anajua kuwa hatma yake baadaye iko nje ya maamuzi yake
Amenukuliwa akisema "Nina furaha, nafurahia maisha hapa na wenzangu katika kikosi. Si maamuzi yangu , Chelsea na Atletico wnapaswa kuongea".
No comments:
Post a Comment