Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers amesisitiza kuwa klabu yake itakuwa ikisaka ubora na sio ujazo wakati atakapo kuwa katika kazi kuboresha kikosi chake wakati wa soko la wachezaji la kipindi cha kiangazi.
Kwasasa wekundu hao wako katika mwendo mzuri wa ushindi baada ya kushinda michezo yao mitatu ya mwisho ya ligi kuu ya England ‘Premier League’ huku Manchester United na Tottenham wakifanya vema kwa kukusanya alama zaidi tangu kuanza kwa mwezi Desemba.
Rodgers anaamini kuwa kuongezeka kwa Daniel Sturridge na Phillippe Coutinho mwezi Januari kumeongeza nguvu na uhai ndani ya kikosi na kusisitiza kuwa ongezeko la wachezaji wenye ubora katika kipindi cha majira ya kiangazi kutarejesha changamoto mpya ya kiushindani zaidi katika nafasi za juu.
"Tunasaka ubora sasa na si uwingi"
"Tunaona matokeo ya ubora wa Coutinho na Sturridge, hicho ndicho tunachokitafuta. Endapo tutawaleta wengine watatu au wanne wa kiwango hicho, tukichanganya na hao tulionao tutakuwa na kikosi cha nguvu ambacho kitaweza kushindana"
Rodgers alivurugwa na jaribio la kumchukua Clint Dempsey kushindikana msimu wa kiangazi uliopita, timu ya utafutaji wa wa wachezaji kitasaidia kuleta wachezaji wa kweli wakati huu.
Anaamini kuwa Liverpool iko sawa katika kila idara na itaendelea kuongeza vipaji.
No comments:
Post a Comment