WAREMBO 31 watakaoshiriki
katika shindano la kuwania taji la Miss Utalii Tanzania 2013, jana walitembelea
katika ofisi za Kampuni ya Uhuru Publications Limited (UPL), inayochapisha
magazeti ya Uhuru, Burudani na Mzalendo. Katika ziara hiyo, warembo hao
walijionea kazi mbalimbali za za utayarishaji wa magazeti hayo, zinavyofanywa na
wafanyakazi wa kampuni hiyo kabla ya kuwafikia wasomaji. Wakizungumza baada ya
ziara hiyo ya mafunzo, warembo hao walisema wamefurahi kutembelea ofisi za UPL
kwa vile ndiyo kampuni pekee kongwe ya habari nchini. Wakati wa ziara hiyo,
Msanifu wa Habari wa gazeti la Uhuru, Lilian Timbuka aliwaeleza warembo hao
kuwa, gazeti la Uhuru lilianzishwa Desemba 9, 1961. Lilian pia aliwaeleza warembo hao kuwa, maktaba ya UPL
ndiyo kongwe kuliko zote nchini na imekuwa ikihifadhi magazeti ya kampuni hiyo
tangu mwaka 1961. "Hata kwa kuzalisha waandishi wa habari nchini, UPL ndio
chimbuko na wanahabari wengi waliopo kwenye vyombo mbalimbali vya habari
nchini," Lilian aliwaeleza warembo hao. Warembo hao ni Rose Edwin, Beatrice Idd,
Sophia Yusufu, Ivony Steven, Irene Thomas, Erica Elibariki, Hamisa Jabir, Debora
Jacob, Jania Abdul, Mulky Huda, Asha Ramadhan, Zena Alkly, Rosemary
Emmanuel. Wengine ni Ana Posialy, Idan John, Doreen Bukoli, Diana
Joachim, Hadija Said, Jesica Peter, Mary Lutta, Halima Hamis, Pauline Mgeni,
Anganile Rodgers, Furaha Kinyunyu, Neema Julius, Chrisina Daudi, Lightness
Kitua, Flora Msangi, Saraphina Jackson, Magreth Michael na Irene Richard.
Shindano la Miss Utalii limepangwa kufanyika Februari 16 mwaka huu kwenye hoteli
ya
Lamada mjini Dar es Salaam.
Lamada mjini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment