Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, January 17, 2013

WAKATI LIGI KUU YA VODACOM IKITARAJIWA KUANZA JANUARI 26, SUPER SPORT YATUMA MAOMBI TFF KUONYESHA MECHI


 Mzunguko wa pili ya Ligi Kuu ya Vodacom unatarajiwa kuanza Januari 26, mwaka huu huku kukiwa na maombi ya televisheni ya SuperSport kuonesha mechi za Super Week kama ilivyokuwa katika mzunguko wa kwanza.
 Raundi tano za awali katika ratiba ya mzunguko wa pili zinabaki kama zilivyo wakati nyingine zilizobaki zitatolewa baada ya kuingiza mechi za Super Week.

 Wakati huo huo, mzunguko wa pili wa Ligi Daraja la Kwanza unatarajia kuanza Januari 26 mwaka huu. Ratiba ya ligi hiyo na tarehe rasmi ya kuanza itatangazwa baada ya kupitiwa na Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inayotarajiwa kukutana mwishoni mwa wiki.

No comments:

Post a Comment