Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, January 7, 2013

WACHEZAJI WA TIMU YA TAIFA "TAIFA STARS" WAKACHA KAMBI YA TIMU HIYO


Kambi ya timu ya taifa ya kujiandaa na michezo ya kirafiki ya Kimataifa imeingia kwenye  siku ya pili leo ikiwa na wachezaji sita tu walioripoti kambini mpaka kufikia leo jioni.

Akiongea jijini Dar es salaam kocha msaidizi wa timu hiyo Sylvester Marsh amesema hali hiyo imetokana na wachezaji wengi kuendelea kuwepo katika timu zao ambazo zimekuwa na majukumu mbalimbali ikiwa ni pamoja na Yanga yenye wachezaji 5 wa timu ya taifa ambao bado wako nchini Uturuki wakiendelea na kambi ya wiki mbili.

Kwa upande wa wachezaji wa Simba wao bado wanaendelea na michuano ya kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar ambapo Mashi amesema wanategemea kuwapata wachezaji hao usiku wa leo na kufanya idadi ya wachezaji 12 idadi ambayo itawawezesha kuanza mazoezi hapo kesho.
  
Kwa upande wa wachezaji wa Azam fc Marsh amesema wanategemea kuwapata hapo kesho kwani wanasubiri mchezo wao wa leo wa michuano ya kombe la Mapinduzi

Kuhusu wachezaji wa Yanga Mashi amesema shirikisho la soka nchini TFF linaendelea na mchakato wa kuwapata wachezaji hao mapema na kwamba wanaimani kuwa wachezaji wa timu ya taifa walioko katika kambi ya Yanga watawahi safari ya Afrika kusini.

Taifa stars ina wachezaji watano kutoka Yanga ambao ni Kelvin Yondan, Frank Domayo, Athumani Iddi Chuji, Simon Msuva na Nadir Haroub Kanavaro.

Kutoka Simba ni Amir Maftaha, Mwinyi Kazimoto, Juma Kaseja, Shomari Kapombe na Amri Kiemba.

Kutoka Azam fc ni Erasto Nyoni, Salum Abubakar, Khamis Mcha, Aggrey Moris, Aishi Manula na John Bocco. 

Wachezaji ambao wamesha ripoti kambini ni pamoja na Juma Kaseja , Issa Rashid, Aggrey Morris, Mbwana Samata, Thomas Ulimwengu na Mrisho Ngasa.

Taifa Stars inataraji kuelekea nchini Ethiopia kwa mchezo wa kimataifa wa kirafiki tarehe 11/01/2013 dhidi ya wawakilishi hao wa kanda ya Afrika mashariki na kati katika fainali za mataifa ya Afrika.  

Kwa vyovyote vile inaonekana kuna uwezekano mdogo wa kambi hiyo ya timu ya Taifa kuwapata wachezaji wa Yanga ambao programu yao mazoezi ya wiki mbili itakamilika mwishoni mwa juma hili. 

Kwa upande wa Simba nao wanajipanga kwa safari ya kuelekea nchini Oman kwa kambi ya maandalizi ya ligi kama ilivyo kwa Yanga ambao wanaendelea na kambi hiyo nchini Uturuki ambapo bila shaka watahitaji kuelekea huko na wachezaji wao wote.

Aidha kwa upande wa Azam yenye dhamira ya kutetea la kombe la mapinduzi hivi sasa wanaendelea vema na michuano hiyo ambapo nao wanataka kuendelea kuwatumia wachezaji wao mpaka fainali endapo watapata nafasi ya kufika katika hatua hiyo ya michuano.

Hata hivyo Marsh anaamini kwa jitihada za TFF watafanikiwa kuwapata wachezaji wote waliotajwa na kocha mkuu wa timu ya taifa Kim Poulsen na kufanikisha programu ya timu ikiwa ni pamoja na kufanikisha safari hiyo ya nchini Ethiopia.

Stars inajiwinda na mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia dhidi ya Morocco mchezo ambao utapigwa Machi.

No comments:

Post a Comment