Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, January 10, 2013

DSTV YAWATAKA WATEJA WAKE KUTOKUWA NA WASIWASI JUU YA VIPINDI VYAO KUFUATIA KUINGIA KWENYE MFUMO WA DIGITALI


Meneja Mahusiano wa Multichoice Tanzania Barbara Kambogi (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Mkurugenzi wa MultiChoice Africa kwa ukanda wa Afrika Mashariki Stephen Isaboke ambapo amesema Wateja wa huduma za Dstv nchini Tanzania wametakiwa kutokuwa na hofu ya kupata muingiliano au kukatika kwa picha katika kipindi hichi cha kutoka analogia kwenda digitali

Barbara Kambogi amesema watanzania ambao wamejiunga na Dstv hawatahitaji kuhama kwa kuwa Dstv iko katika mfumo wa digital tangu awali
Ameoneza kuwa Dstv imekuwa ikitoa huduma za digital televisheni kwa Tanzania kwa kipindi cha miaka 17 iliyopita, ambapo wateja wake wameweza kupata channel nyingi zaidi za kuchagua zikiwa na picha safi na sauti bora.
Kupitia vifurushi tofauti vinavyotolewa na Dstv wateja wanakuwa na maamuzi ya kuchagua kifurushi anachotaka na bei ambapo Ofa ya msimu wa Sikukuu za Krismas inaendelea pamoja na punguzo la asilimia 10 la kufanya malipo kabla ya muda uliolipia huduma kumalizika. Kulia ni Operation Manager wa Multichoice Tanzania Bw. Ronald Baraka Shelukindo.

Operation Manager wa Multichoice Tanzania Ronald Baraka Shelukindo akifafanua jambo kuhusu Televisheni nyingine kuingizwa katika huduma za DStv na kusema suala hilo litategemeana na makubaliano na mikataba na wamiliki pamoja na kutegemea uwezo wa Satelite.
Kwa Tanzania DStv inamkataba na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) la kuichukua TBC katika DStv Platform ambapo itakuwa inaonekana bure hata kama hujalipia king’amuzi chako chaneli hiyo haikatwi.
Bw. Shelukindo amewataka Watanzania kuendelea kununua ving’amuzi vya DStv kabla ya kuisha kwa Ofa ya msimu wa Sikukuu za Krismas na Mwaka mpya.

No comments:

Post a Comment