Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, January 23, 2013

AZAM FC YAMALIZA ZIARA YAKE KENYA KWA KUIFUNGA KCB

Azam FC yamaliza ziara na ushindi, L-W-W
Timu ya Azam Fc ambayo inajiandaa na michuano ya Kombe la Shirikisho na ligi kuu Tanzania Bara, imemaliza ziara yake nchini Kenya kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya KCB.

Kwa matokeo hayo Azam inatoka na rekodi huko ya L-W-W (L-Loose, W-Win)
Mchezo huo ulichezwa jana, Goli pekee la Azam FC katika mchezo huo lilifungwa na Ibrahim Mwaipopo

Hapo kabla golikipa kinda toka Azam Academy ambaye pia huitwa kikosi cha timu ya Taifa Stars Aishi Salum Manula alikuwa shujaa langoni mwa Azam FC katika mchezo wao dhidi ya Sofapaka katika ushindi wa 1-0 dhidi ya timu hiyo.

Katika mchezo huo Azam ilipata bao moja kwa njia ya penati kupitia mshambuliaji wake Gaudence Mwaikimba kipindi cha kwanza
Huu ulikuwa mchezo wa tatu kwa Azam FC baada ya kupoteza mchezo wa kwanza 2-1 dhidi ya AFC Leopards

No comments:

Post a Comment