Wednesday, January 23, 2013
KABANGE TWITE KUKOSA USAJILI YANGA YAITUPIA TFF LAWAMA
Sakata la mchezaji Kabange Twite kukosa cheti cha uhamisho wa Kimataifa(ITC) limechukua sura mpya baada ya klabu ya Yanga kulitwika mzigo Shirikisho la Soka Tanzania(TFF) kuwa ndiyo chanzo cha mkasa huo.
Jana TFF ilitangaza orodha ya wachezaji waliosajiliwa na klabu mbalimbali za ligi kuu lakini bila ya kuwamo kwa jina la Kabange ambaye Yanga ilimsajili kwaajili ya msimu ujao.
Katibu Mkuu wa Yanga Laurence Mwalusako alisema kuwa klabu yake imeiachia TFF ishughulikie suala hilo kwa madai kuwa ndiyo iliyotuma Shirikisho la Soka la Dunia (FIFA) taarifa za usajili wa mchezaji huyo nje ya muda unaotambulika .
“Sisi kama Yanga tulikamilisha ndani yamuda taratibu zote za usajili wa Kabange lakini TFF ndiyo waliochelewa kutuma taarifa zake Fifa baada ya kukuta ‘System haiko Active’,”alisema Mwalusako na kuongeza:
“Nataka ieleweke hivyo kwamba suala hili linashughulikiwa na TFF ambao ndiyo wanawasiliana na Fifa itakapotumwa tutamtumia kwani bado ni mchezaji halali wa Yanga licha ya kwamba ITC yake haijapatikana,”.
Mwalusako alisema kuwa,klabu yake ina matumaini kuwa Fifa itatuma kwa wakati ITC ya mchezaji huyo kwakua kama klabu haikufanya uzembe wowote katika kukamilisha taratibu za usajili.
Ofisa habari wa TFF Boniface Wambura akizungumzia suala hilo alisema kuwa Shirikisho lake halijapokea jina la Kabange Twite ,hivyo ilikuwa inasubiri kibali kutoka Fifa.
“Hatuna jina la Kabange ambaye kwa mujibu wa Yanga amesajiliwa wakati wa usajili wa dirisha dogo,suala lake liko ndani ya Fifa.
“Yanga na Fifa wanaweza kukaa meza moja na kumalizana kwani uhamisho wake ulichelewa na sisi hatukuwa na uwezo kumwidhinisha kucheza Yanga,”.alisema Wambura
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment