Mshambuliaji Hassan Rashid Yanga B akijaribu kugeuka na mpira kwenye mchezo mashindano ya uhai uliochezwa leo asubuhi uwanja wa Karume huku beki Twalib Kiburuma wa Kagera Sugar akimdhibiti |
TIMU ya Yanga B leo asubuhi iliifunga Kagera Sugar B mabao 6-2 kwenye mashindano ya Uhai, mchezo uliochezwa uwanja wa Karume
Mchezo huo ambao unaweza kusema kipindi cha kwanza ulikuwa wa upande mmoja ulishuhudia Yanga B wakienda mapumziko wakiongoza kwa mabao 4-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko hali iliyofanya Kagera Sugar kubadilika kwani waliweza kushambulia na kuzuia.
Mabao ya Yanga yalifungwa na George Banda dakika ya nne na 22, Clever Mkini dakika ya 15 na 49, Abdallah dakika 42 na karamu ya mabao ilifungwa na Rehan Rehan dakika ya 78
Kagera Sugar ambayo inaundwa na wachezaji wenye miili iliyojengeka walijipatia mabao yake kupitia kwa Twalib Kiburuma dakika ya 60 na Aron Bareko dakika ya 64.
Yanga ambayo kwenye michezo miwili iliyotangulia ilifungwa mmoja na kutoka sare mmoja imeonyesha nia ya kutaka kuingia robo fainali baada ya ushindi wa leo kwani imefikisha ponti 4 nyuma ya JKT Oljoro wenye pointi 6 na mchezo mmoja mkononi.
Akizungumza na MTANZANIA baada ya mchezo kumalizika Mwenyekiti wa soka la vijana Alhaj Msafiri Mgoyi alisema anashukuru kuona timu za mikoani zikileta changamoto kwenye mashindano haya.
"Imezoeleka timu za Dar es Salaam ndio zina uwezo wa kushinda lakini kwenye uhai mwaka huu timu za mikoani zipo vizuri na zinaonyesha vipaji halisi" alisema Mgoyi.
No comments:
Post a Comment