Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, December 16, 2012

UCHAGUZI WA TWFA KUFANYIKA MIDLAND HOTELI MOROGORO

UCHAGUZI wa chama cha soka la wanawake Tanzania (TWFA) unatarajiwa kufanyika Desemba 19 mwaka huu, kwenye hoteli ya Midland mjini Morogoro huku mikoa sita ikiwa kwenye hati hati ya kutoshiriki.

Kwa mujibu wa taarifa ya TWFA, mikoa hiyo ambayo ni wanachama wa Chama cha Soka ya Wanawake Tanzania (TWFA) hawatashiriki kwa vile hadi sasa haijapokea taarifa za uchaguzi kwenye vyama hivyo.

Vyama hivyo ni vya mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Mbeya, Rukwa, Shinyanga na Tabora.

Wagombea wanaotarajiwa kupigiwa kura nafasi ya mwenyekiti kwenye uchaguzi huo ni Isabela Kapera, Joan Minja na Lina Kessy na makamu mwenyekiti ni Rose Kissiwa.

Amina Karuma na Cecilia Mkafum nafasi ya Katibu Mkuu, Zena Chande nafasi ya Mjumbe Mkutano Mkuu wa TFF na Sophia Charles na Triphonia Temba wanaowania ujumbe wa Kamati ya Utendaji.

No comments:

Post a Comment