Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, November 10, 2012

MABONDIA WA TANZANIA WADUNDWA NA WENZAO WA ZAMBIA

Bondia Kassim Hussein (aliyevaa nyekundu)  wa Tanzania a kikwepa konde la Bondia Charles Lumbwe wa Zambia (aliyevaa bluu) alloimrushia  kwenye mchezo wa kirafiki kg 64 ulichezwa kwenye ukumbi wa DDC Kariakoo

Bondia Kassim Hussein (aliyevaa nyekundu)  wa Tanzania akijapanga jinsi ya kupiga ngumi zenye uzito mpinzani wake Bondia Charles Lumbwe wa Zambia (aliyevaa bluu)   kwenye mchezo wa kirafiki kg 64 ulichezwa kwenye ukumbi wa DDC Kariakoo

Bondia Mohamed Chimbumbui wa Tanzania (aliyevaa nyekundu) na Mbachi Kaonga wa Zambia ( aliyevaa blue) wakipanga jinsi ya kushambulia kwenye mpambano wa kg 75 wenye raundi tatu, Mohamed alipigwa kwa TKO raundi ya pili

Bondia Mohamed Chimbumbui wa Tanzania (aliyevaa nyekundu) akizuia ngumi nzito za Mbachi Kaonga wa Zambia kg 75


MABONDIA wa ngumi za Ridhaa wa Tanzania leo wamechezea kichapo baada ya kupigwa michezo minne kati ya mitano iliyochezwa leo na mabondia toka Zambia kwenye ukumbi wa DDC Kariakoo

Mapambano haya ambayo yalikuwa ni ya kirafiki yenye raundi tatu ilishuhudia Said Hofu akifungua pazia (kg 49) kwa kupigwa kwa pointi na Caristo Bwalia toka Zambia

Mpambano wa pili kg 56 ulishuhudia Frank Nicolaus wa Tanzania akipigwa na Russel Mwamba wa Zambia kwa pointi pia.

Kg 60 ndipo mtanzania Ismail Galiatano alimshushia ngumi nzito nzito John Chimpwele wa Zambia na kusababisha kuchanika juu ya jicho na kutokwa damu nyingi ndipo mwamuzi alisimamisha mchezo na kumpa ushindi Ismail Galiatano.(RSC)

Mpambano wa nne kg 64 Mtanzania Kassim Hussein alipokea kipigo toka kwa  Charles Lumbwe kwa kupigwa kwa pointi.

Funga kazi kg 75 ikawa ndio usiseme maana Mohamed Chimbumbui alipigwa kwa TKO na Mbachi Kaonga wa Zambia baada ya kumsukumizia makonde mazito mazito na kushindwa kuyahimili na kujikuta akianguka kila mara.

Katibu wa Chama ngumi za ridhaa, Makore Mashaga alisema wamepoteza mpambano huo lakini anashukuru wamepata mazoezi ya kujiandaa na mashindano ya ndano yanayotarajiwa kuanza Novemba 26 kwenye uwanja wa ndani wa taifa, jijini Dar es salaam.

Mabondia watanzania walisema kupigwa kwao kunatokana na maandalizi hafifu waliyopata na mashindano kuahirishwa mara kwa mara pia kuliwafanya morali kushuka.

Naye Katibu wa Ngumi za Ridhaa wa Zambia Lut. Kanali Man Muchimba amesema amefurahi kucheza na watanzania kwani wamepata mazoezi ya kuwasaidia kucheza mashindano ya kanda ya tano yatakayofanyika nchini kwao mapema Desemba.

No comments:

Post a Comment