Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, November 12, 2012

ARUSHA BINGWA SLAM SPRITE

Mabingwa kikapu, timu ya mkoa wa Arusha wakikabidhiwa zawadi ya kombe na Katibu Mkuu wa Shirikisho la mpira wa kikapu (TBF) Michael Maluwe, kwenye uwanja wa ndani wa taifa jana baada ya kuifunga Dodoma vikapu 11 kwa 8.

Mabingwa wa kikapu wa timu ya mkoa wa Dodoma (wachezaji 3+3) wakikabidhiwa zawadi ya ngao na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa kikapu (TBF) Michael Maluwe, kwenye uwanja wa ndani wa taifa janabaada ya kuifunga Arusha vikapu 10 kwa 5



TIMU ya kikapu ya mkoa wa Arusha jana  iliibuka ubingwa wa Slam Sprite baada ya kuifunga Dodoma kwa vikapu 11 kwa 8.

Mashindano hayo ambayo yalianza kuchezwa mikoani yameweza kuibua vipaji vingi ambavyo vitakuwa tunu kwa taifa.


Awali akizungumza, Katibu wa Shirikisho wa Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Michael Maluwe, aliishukuru Kampuni ya Cocala kupitia kinywaji chake cha Sprite kwa kufanikisha mashindano.

Maluwe alisema kupitia kampuni hiyo wameweza kuona nyota ambao watalisaidia taifa kwenye mashindano mbalimbali ndani na nje ya nchi.

"Makampuni mengine yaige mfano kwa Copa Cocala ili kuinua michezo Tanzania", alisema.

Arusha iliibuka bingwa kwenye mchezo wa wachezaji watano na kupewa kombe, fulana na kofia huku Dodoma wao wakiondoka na Ipod kila mchezaji,fulana na kofia.

Kwenye mchezo wa wachezaji watatu kila timu Dodoma iliifunga Arusha vikapu 10 kwa 5 na kufanikiwa kutwaa ngao, fulana na kofia na Arusha kila mchezaji kuondoka na ipod, kofia na fulana.

Kwa upande wa street dancing mkoa wa Kilimanjaron walishinda na kupewa ngao.

Mikoa ambayo ilishiriki katika mashindano hayo ni Arusha, Dodoma, Kilimanjaro, Mwanza, Mbeya pamoja na Dar Es Salaam.

Mkoa wa Dar es salaam hakuweza kufurukuta kwani uliondolewa kwenye makundi kwa kufungwa na Kilimanjaro vikapu 15 kwa 11 na baadae kupotea kabisa baada ya kufungwa na Dodoma vikapu 28 kwa 12.

No comments:

Post a Comment