KAMATI ya Uchaguzi ya Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA) imeongeza muda kwa wagombea kuchukua fomu kwa ajili ya uchaguzi wa chama hicho ambao unatarajiwa kutafanyika Novemba 25 mwaka huu.
Akizungumza na wandishi wa habari, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TAFCA, Ramadhan Mambosasa, alisema kuwa jana ndiyo ilikuwa mwisho wa kuchukua fomu lakini mwitikio wa wagombea bado umekuwa mdogo kwani ni watano tu waliojitokeza.
Hivyo, amesema wameongeza muda wa kuchukua na kurudisha fomu na mwisho itakuwa ni Oktoba 19 mwaka huu saa 10 kamili alasiri.
Alisema fomu zinapatikana ofisi za TAFCA zilizoko Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.
Nafasi zinazogombewa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF, Mhazini na wajumbe watatu wa Kamati ya Utendaji.
Mambosasa amewataka wanachama wa TAFCA kutumia fursa yao kikatiba kwa kuchukua fomu ili wapate nafasi ya kukiongoza chama ili uchaguzi ufanyike tarehe iliyopangwa.
No comments:
Post a Comment