MWAMUZI Mathew Akrama kutoka jijini Mwanza ameteuliwa kuchezesha pambano la watani wa jadi la Simba na Yanga litakalofanyika keshokutwa katika Uwanja wa Taifa huku taarifa zikieleza kwamba ni muumini wa dhehebu la kilokole.
Taarifa kutoka kwa rafiki wa
karibu wa mwamuzi huyo zinasema kwamba Akrama ni muumini mzuri wa kanisa la
kilokole huku akitumia muda wake wa ziada anaupata nje ya uamuzi katika
uimbaji.
“Akrama ni muumini mzuri wa
kanisa la kilokole la EAGT na ni mtu wa kazi hawezi kupokea rushwa hata kidogo kutokana
na msimamo wake kidini.
“Kwa msimamo wake ni dhahiri
kwamba maamuzi yake yanaweza kuwa bora na tofauti na yale tunayoyaona katika
baadhi ya viwanja kwa hiyo katika hili hakuna tatizo,” alisema rafiki huyo
ambaye kitaaluma ni mwamuzi pia.
Jana, Ofisa Habari wa Shirikisho
la soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura alisema kuwa Akrama atakuwa mwamuzi wa
kati wa pambano hilo ambalo linaendelea kuvuta hisia za mashabiki wa soka ndani
na nje ya mipaka ya Tanzania.
“ Akrama atasaidiwa na Samuel
Mpenzu kutoka Arusha na Ephrony Ndissa wa Dar es Salaam huku mwamuzi wa mezani
ni Oden Mbaga kutoka Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment