Kamati
ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ilikutana Oktoba 5 mwaka huu kupitia na kufanya uamuzi katika masuala mbalimbali
na kupanga Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ianze kutimua vumbi Oktoba 20
mwaka huu.
Timu
zimepangwa katika makundi matatu ya timu nane nane ambapo zitacheza
ligi hiyo kwa mtindo wa nyumbani na ugenini. Mshindi wa kila kundi ndiye
atakayepata tiketi ya kucheza Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu ujao
wakati timu ya mwisho kila kundi itashuka daraja kurudi Ligi ya Mkoa.
Kundi
A lina timu za Burkina Moro ya Morogoro, Kurugenzi Mufindi ya Iringa,
Majimaji ya Songea, Mbeya City ya Mbeya, Mlale JKT ya Ruvuma, Mkamba
Rangers ya Morogoro, Polisi Iringa na Small Kids ya Rukwa.
Ndanda
FC ya Mtwara, Ashanti United, Green Warriors, Moro United, Polisi,
Tessema, Transit Camp na Villa Squad zote za Dar es Salaam ndizo
zinazounda kundi B wakati kundi C ni Kanembwa JKT ya Kigoma, Morani ya
Manyara, Mwadui ya Shinyanga, Pamba ya Mwanza Polisi Dodoma, Polisi
Mara, Polisi Tabora na Rhino Rangers ya Tabora.
Ada
ya ushiriki wa ligi ni sh. 200,000 zinazotakiwa kulipwa kabla ya Oktoba
13 mwaka huu. Pia Oktoba 13 mwaka huu kutakuwa na kikao kati ya
wenyeviti wa klabu zote zinazoshiriki ligi hiyo na Kamati ya Ligi ambapo
pia itafanyika draw (ratiba).
No comments:
Post a Comment