Kamati
ya Ligi imesogeza mbele kwa siku moja mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati
ya Kagera Sugar na Yanga iliyokuwa ichezwe Oktoba 7 mwaka huu
mjini Bukoba kutokana na Uwanja wa Kaitaba kuwa na shughuli nyingine za
kijamii.
Sasa
mechi hiyo itachezwa Oktoba 8 mwaka huu kwenye uwanja huo
huo. Mabadiliko hayo pia yameathiri mechi kati ya Toto Africans na Yanga
iliyokuwa ichezwe Oktoba 10 mwaka huu Uwanja wa CCM Kirumba jijini
Mwanza. Mechi hiyo sasa itachezwa Oktoba 11 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment