KIKOSI CHA SIMBA |
Mshambuliaji wa SIMBA Christopher Edward |
TIMU ya Simba leo majira ya saa 11 jioni itacheza na Prison ya Mbeya uwanja wa Taifa bila mshambuliaji wao wa kimataifa toka Uganda Emanuel Okwi ambaye anatumikia adhabu yake ya kadi nyekundu aliyoonyeshwa kwenye mchezo dhidi ya JKT Ruvu.
Okwi alimpiga kiwiko Kessy Mapande wa JKT Ruvu wakati mpira ukiwa haupo mchezo hivyo. Kufuatana na sheria za soka, sheria namba 12 ambayo inasema tabia mbaya mchezoni kwenye makosa makubwa saba ambayo mchezaji anaonyeshwa kadi nyekundu Okwi alifanya kosa ambalo lipo kwenye violet conduct na kufuatana na sheria alipashwa kukosa mechi mbili tu lakini kanuni zinazoendesha ligi ya Tanzania zimeongeza adhabu kuwa mechi tatu na faini
Pia mshambuliaji huyo atakosa mchezo wa Simba na Yanga utakaochezwa Octoba 3 mwaka huu uwanja wa Taifa.
Washambuliaji chipukizi wa Simba Shomari Kapombe na Christopher Edward wamewatoa wasiwasi mashabiki kwa kusema wao wakae mkao wa kukesha siku hiyo maana wataleta furaha Msimbazi kwa kuhakikisha wanatoka na pointi 3.
Washambuliaji hawa wamekuwa ndio habari ya mjini kwa sasa kutokana na kandanda wanalosakata kuwa lakiustadi zaidi
No comments:
Post a Comment