Serengeti boys wakiwa mazoezi Karume kabla ya kuondoka kwenda Mbeya |
TIMU ya vijana U-17 Serengeti boys jana ilipata kipigo cha bao 1-0 toka kwa Mbozi United ya mkoa wa Mbeya kwenye mchezo wa kirafiki.
Bao pekee la Mbozi lilifungwa na Awadhi Richard baada ya kutokea piga ni kupige langoni mwa Serengeti.
Serengeti boys ambayo ipo Mbeya kwa mwaliko wa Chama cha soka manispaa ya Mbeya (MUFA) ilikumbana na kipigo hicho ikiwa na kumbukumbu ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Prison ambayo inashiriki ligi kuu mchezo uliochezwa mji wa Nakonde mpakani mwa Zambia na Tanzania.
Serengeti Boys leo jioni inatarajia kucheza mechi nyingine na Mbeya City ambao ni mchezo wa tatu wakiwa jijini Mbeya.
Timu hii inajiandaa na mashindano ya vijana ya Afrika yanayotarajiwa kufanyika mwakani nchini Morocco na inatarajia kucheza mchezo wa raundi ya pili na vijana wenzao wa Misri Octoba 14, mwaka huu jijini Dar es salaam.
Kwa mujibu wa Kocha wa timu hiyo, Jakob Michelsen kambi hiyo inaendelea vizuri, na anatarajia kupata mechi moja ya kirafiki ya kimataifa kabla ya kucheza mechi ya mashindano na Misri.
No comments:
Post a Comment