Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, September 17, 2012

RAJABU MAOJA APANIA MAKUBWA NAMIBIA IBF

BONDIA Rajabu Maoja amejinadi kuhakikisha anarudi na ushindi katika pambano lake na ubingwa wa IBF dhidi ya Mnamibia, Gottlieb Ndokosho katika pambano  linalotarajiwa kufanyika Septemba 29, mwaka huu katika jiji la Windhoek, Namibia.

Akizungumza kwa njia ya simu akiwa mkoani Tanga, alikoweka kambi, Maoja alisema, katika pambano hilo lililopewa jina la ‘Vita ya jangwa la Kalahari’ amejipanga kuhakikisha anawapa raha Watanzania kwa kurudi na ubingwa kwani ana imani atarudi nao.

“Nipo Tanga ambapo nyumbani lakini pia ndipo nilipoweka kambi yangu hadi siku nitakayokwenda katika shindano, nimejipanga kuhakikisha nanyakua ubingwa ikiwa ni pamoja na kuitangaza nchi kwani rekodi yangu ni nzuri tofauti na ya mpinzani wangu na nimejiandaa vizuri tangu nipate taarifa ya pambano hili,” alisema.

Pambano hilo litasimamiwa na rais wa IBF katika Bara la Afrika, Mashariki ya Kati, Ghuba ya Uarabuni na Ghuba ya Uajemi, Onesmo Ngowi akishirikiana na Bodi ya Ngumi na Mieleka ya Namibia.

Kwa upande wake Ngowi alisema, mapambano hayo yanatambuliwa na IBF yapo katika mpango wa programu ya ‘Utalii wa michezo’ ambao IBF na USBA umeufadhili na kuuendesha katika bara la Afrika huku Tanzania na Ghana zikiwa ni nchi za majaribio katika mpango huo.

Aliongeza kuwa programu hiyo, itawapa mabondia wengi wa Kitanzania nafasi nyingine ya kugombea mkanda wa IBF sehemu mbalimbali duniani na kuitangaza Tanzania.

No comments:

Post a Comment